A great place to access the latest news and information.

Breaking

Post Top Ad

Your Ad Spot

Friday, September 15, 2017

Tigo Yatoa Zawadi kwa Washindi wa Promosheni ya ‘Nunua Simu na Ushinde.



 Meneja Mawasiliano wa Tigo, Woinde Shisael (kulia), akikabidhi fungua ya Pikipiki  aina ya Hero  kwa Pius Kavike, mmoja kati ya washindi nane (8) waliojishindia pikipiki nne  pamoja na televisheni   nne za LED flati skrini  kwenye promosheni ya Nunua Simu ya Tecno R6,S1 na Ushinde, Makabidhiano hayo yamefanyika Makao Makuu ya Tigo jijini Dar es Salaam leo.

Meneja Mawasiliano wa Tigo, Woinde Shisael, akiongea na waandishi wa habari wakati akikabidhi zawadi kwa washindi waliojishindia pikipiki nne  pamoja na televisheni   nne za LED flati skrini  kwenye Promosheni ya Nunua Simu ya Tecno R6,S1 na Ushinde, Makabidhiano hayo yamefanyika Makao Makuu ya Tigo jijini Dar es Salaam leo
.
Meneja Mawasiliano wa Tigo, Woinde Shisael (kulia), akikabidhi fungua ya Pikipiki  aina ya Hero  kwa Tumaini Massra, mmoja kati ya washindi nane (8) waliojishindia pikipiki nne  pamoja na televisheni   nne za LED flati skrini  kwenye promosheni ya Nunua Simu ya Tecno R6,S1 na Ushinde, Makabidhiano hayo yamefanyika Makao Makuu ya Tigo jijini Dar es Salaam leo.


Tigo Yatoa Zawadi kwa Washindi wa Promosheni ya ‘Nunua Simu na Ushinde.”

Wateja wajinyakulia pikipiki 4 na televisheni 4 za LED  katika droo ya wiki hii.


Dar es Salaam,  Septemba15, 2017- Kampuni inayoongoza kwa mageuzi ya kidigitali nchini, Tigo Tanzania, leo imetoa pikipiki nne (4) na televisheni nne (4) za LED flatscrini kwa washindi wa promosheni yake inayoendelea nchini nzima ya ‘Nunua Simu na Ushinde’.

Akizungumza katika hafla ya kukabidhi zawadi kwa washindi iliyofanyika katika ofisi za Tigo, jijini Dar es Salaam leo, Meneja Mawasiliano wa Tigo, Woinde Shisael aliwatangaza washindi wa pikipiki kuwa ni Tumaini Massra (kinyozi) na Pius Kivike (fundi) wa Dar es Salaam, Restituta Gervas wa Mwanza na Moses William wa Sumbawanga. Washindi wa wiki hii wa luninga za LED flatscrini ni Bahati Sambayuka wa Dar es Salaam, Venanty Ndunguru wa Mtwara, Jackson Mwenga wa Mbeya na Amuri Kalinga wa Iringa.

Akiwapongeza washindi, Woinde alisema kuwa Tigo inaongoza katika mageuzi ya kidigitali nchini na ndio maana inawapa wateja wake fursa ya kumiliki simu bora za kisasa kwa bei nafuu, pamoja na kuwapa nafasi ya kushinda zawadi zitakazoboresha maisha yao.

‘Huu ni muendelezo wa juhudi za Tigo kukuza mabadiliko ya digitali nchini. Kwa manunuzi ya simu aina ya Tecno S1 na Tecno R6 kutoka maduka yote ya Tigo nchini, wateja wanaingizwa kwenye droo inayowapa nafasi ya kushinda mojawapo ya pikipiki 14 na televisheni 14 za kisasa ambazo bado zinazoshindaniwa kwenye promosheni hii,’ aliongeza.

Promosheni hii ya Tecno S1 na Tecno R6 inahusu tu wale wateja watakaonunua simu za aina hii kutoka kwa maduka ya Tigo nchini kote. Simu ya Tecno S1 ni ya mfumo wa 3G na inapatikana kwa bei ya shilingi 99,000/- tu. Simu ya Tecno R ni ya mfumo wa 4G na inapatikana kwa bei ya shilingi 195,000/- tu.

‘Simu zote mbili ni za kisasa na zina uwezo wa kutumia mfumo wa data, kwa hiyo wateja wataweza kutumia huduma bora za data za 3G na 4G kutoka Tigo, hii ikiwa inalingana na aina ya simu watakayonunua’ Woinde alifafanua.
...........................................................................................................................
Kuhusu Tigo:

Tigo Tanzania ni kampuni ya simu inayotoa huduma bora za maisha ya kidigitali nchini Tanzania. Tigo ilianza kuendesha shughuli zake nchini Tanzania mwaka 1994.

Kupitia huduma zake za kipekee za sauti, ujumbe mfupi, intaneti yenye kasi na huduma za kifedha kupitia simu za mikononi, Tigo inaongoza kwa ubunifu wa kidigitali kwa kuwa kampuni ya kwanza Tanzania kuzindua facebook na smartphone zenye lugha ya Kiswahili, huduma ya TigoPesa, pamoja na huduma ya kwanza inayowezesha wateja kufanya miamala ya fedha kupitia simu za mkononi kwenda nje ya nchi yenye uwezo wa kubadili thamani ya fedha kwa sarafu ya nchi husika Afrika Mashariki.   
  
Tigo ni kampuni ya pili kwa ukuwa nchini na imekuwa kampuni ya simu inayokuwa kwa kasi zaidi nchini kwa kipindi cha miaka mitatu mfululizo. Kupitia mkakati mkubwa wa kupanua na kuboresha huduma zake, kati ya mwaka 2015 hadi 2016, Tigo  ilizindua mtandao wa 4G LTE jijini Dar es Salaam na katika miji mingine 22 nchini.

Tigo inajivunia jumla ya watumiaji milioni 10 wa simu waliosajiliwa, na imetoa nafasi za ajira za moja kwa moja na zile zisizokuwa na moja kwa moja kwa Watanzania wapatao 300,000; hii ikiwa ni pamoja na wawakilishi wa huduma kwa wateja, wafanyabiashara wakubwa wa fedha kupitia simu za mikononi, mawakala wa mauzo na wasambazaji. 
 
Tigo ni nembo ya kibiashara ya Millicom, kampuni ya kimataifa inayoongoza mageuzi ya maisha ya kidigitali katika nchi 13 duniani. Ikiwa inaendesha shughuli zake za kibiashara katika bara la Afrika na Amerika ya Kusini, Ofisi kuu za Millicom zipo Ulaya na Marekani.
………………………………………………………………………………………………………

Kwa taarifa zaidi tembelea: www.tigo.co.tz au wasiliana na: 
Woinde Shisael – Meneja Mawasiliano
Simu: +255 713 123431            Barua pepe: Woinde.shisael@tigo.co.tz



No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages