Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mama Samia Suluhu Hassan (kushoto), akikaribishwa na Mwenyekiti wa Bodi ya NBC, Nehemiah Machechu katika sherehe za maadhimisho ya miaka 50 ya Benki jijini Dar es Salaam juzi. Wa pili kushoto ni Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Dk. Ashatu Kijaji na Meneja Mahusiano wa NBC, William Kallaghe (kulia).
Makamu wa Rais, Mama Samia Suluhu Hassan akisalimiana na Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Job Ndugai (kushoto), katika sherehe za maadhimisho ya miaka 50 ya Benki ya NBC jijini Dar es Salaam juzi. Wengine kutoka kulia ni Waziri Mkuu wa zamani, Dk. Salim Ahmed Salim na Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Dk. Ashatu Kijaji.
Makamu wa Rais, Mama Samia Suluhu Hassan (katikati), akipiga picha ya pamoja na kutoka kushoto; Mjumbe wa Bodi ya NBC, Dk. Kassim Hussein; Spika, Job Ndugai; Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Dk. Ashatu Kijaji; Mwenyekiti wa Bodi ya NBC, Nehemiah Mchechu; Naibu Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Dr. Bernard Kibesse na Waziri Mkuu wa zamani, Dk. Salim Ahmed Salim.
Meneja Mahusiano wa Benki ya NBC, William Kallaghe (kulia), akiwaongoza Makamu wa Rais, Mama Samia Suluhu Hassan (katikati) na Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Dk. Ashatu Kijaji (kushoto), walipokwenda katika sherehe za maadhimisho ya miaka 50 ya benki hiyo ambapo makamu wa rais alikuwa mgeni rasmi. Wa pili kulia ni Mwenyekiti wa Bodi ya NBC, Nehemiah Mchechu. Sherehe hizo zilifanyika jijini Dar es Salaam juzi.
Meneja Mahusiano wa NBC, William Kallaghe akitoa maelezo kwa njia ya picha kwa Makamu wa Rais, Mama Samia Suluhu Hassan (wa tatu kulia), kuhusu historia ya benki hiyo tokea ilipoanzishwa wakati wa sherehe hizo. Wa pili kulia ni Mwenyekiti wa Bodi ya benki hiyo, Nehemiah Mchechu na Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Dk. Ashatu Kijaji.
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa NBC, Theobald Sabi akizungumza katika hafla hiyo.
Mwenyekiti wa Bodi ya NBC, Nehemiah Mchechu akizungumza katika sherehe hizo.
Spika wa Bunge ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Job Ndugai akizungumza.
Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Dk. Ashatu Kijaji akizungumza.
Mheshimiwa Makamu wa Rais, Mama Samia Suluhu Hassan akihutubia katika sherehe za maadhimisho ya miaka 50 ya Benki ya NBC jijini Dar es Salaam juzi.
Mwenyekiti wa Bodi ya NBC, Nehemiah Mchechu akikabidhi zawadi kwa Makamu wa Rais, Mama Samia Suluhu Hassan.
Makamu wa Rais, Mama Samia Suluhu Hassan (katikati), akimkabidhi zawadi Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Dk. Ashatu Kijaji katika sherehe za maadhimisho ya miaka 50 ya Benki ya NBC jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Mwenyekiti wa Bodi ya NBC, Nehemiah Mchechu.
Makamu wa Rais, Mama Samia Suluhu Hassan (kulia), akimkabidhi zawadi kwa Arnold Kilewo mmoja wa viongozi wa bodi ya zamani ya NBC katika hafla hiyo. Katikati ni Mwenyekiti wa Bodi ya NBC, Nehemiah Mchechu.
Mwanamuziki mashuhuri wa Afrika Kusini, Yvonne Chakacha (kulia), akisakata rumba na Mkurugenzi Mtendaji wa NBC Tanzania, Theobald Sabi katika sherehe za maadhimisho ya miaka 50 ya Benki ya NBC jijini Dar es Salaam.
Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Dk. Ashatu Kijaji akiagana na Mjumbe wa Bodi ya NBC, Dk. Kassim Hussein mara baada ya sherehe za maadhimisho ya miaka 50 ya benki hiyo jijini Dar es Salaam. Wa pili kushoto ni Mwenyekiti wa Bodi ya NBC, Nehemiah Mchechu, Meneja Mahusiano, William Kallaghe (kulia) na Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa benki hiyo, Theobald Sabi.
Mwanamuziki mashuhuri wa Afrika Kusini, Yvonne Chakacha (kushoto), akitoa burudani katika sherehe za maadhimisho ya miaka 50 ya Benki ya NBC hiyo jijini Dar es Salaam juzi.
Mkurugenzi Mtendaji wa zamani wa NBC, Lawrence Mafuru (kulia) akisalimiana na viongozi wa NBC, kutoka kushoto, Kaimu Mkurugenzi Mtendaji, Theobald Sabi,Ofisa Fedha Mkuu wa NBC, Jaffari Matundu na Mkurugenzi wa Wateja Binafsi, Filbert Mponzi.
No comments:
Post a Comment