A great place to access the latest news and information.

Breaking

Post Top Ad

Your Ad Spot

Tuesday, September 19, 2017

RC MAKONDA: KUZINDUA RASMI UJENZI WA OFISI ZA WALIMU

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda, wa tatu (kushoto) akikata utepe kuashiria uzinduzi rasmi wa ujenzi wa ofisi 402 za walimu katika  Mkoa wake, uzinduzi huo umefanyika katika viwanja vya Gereza la Ukonga jijini hapa leo, wapili (kushoto) ni Mwenyekiti wa kamati ya ujenzi wa ofisi hizo Kanali Charles Mbuge, na wengine ni baadhi ya wajumbe wa kamati hiyo.  
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda, akizungumza na waandishi wa habari wakati wa uzinduzi rasmi wa ujenzi wa ofisi 402 za walimu katika  Mkoa wake, uzinduzi huo umefanyika katika viwanja vya Gereza la Ukonga jijini hapa leo, wapili (kushoto) ni Mwenyekiti wa kamati ya ujenzi wa ofisi hizo Kanali Charles Mbuge, na wengine ni baadhi ya wajumbe wa kamati hiyo.  
Mwenyekiti wa kamati ya ujenzi wa ofisi 402 za walimu Mkoa wa Dar es Salaam, Kanali Charles Mbuge, akizungumza katika hafla hiyo.


 Makonda akisalimiana na wajumbe wa kamati ya ujenzi







 


Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Paul Makonda amezindua  rasmi ujenzi wa ofisi za walimu 402 kwa Mkoa  huo, huku akiwataka wananchi na wadau  wengine kuunga mkono jitihada hizo.

Makonda ameyasema hayo leo alipotembelea  katika eneo ambalo limetengwa  maalumu kwa shughuli za ufyatuaji wa tofali  Ukonga Magereza jijini humo.


"wenzetu waliwahi kupanga lakini hawakuweza kufanikisha suala hili la ujenzi ,lakini sisi hatutakubali kushindwa lazima tutafika mwisho tukiwa na matokeo mazuri"alisema Makonda.

Amesema watahakikisha ndani ya wiki hii inapatikana mifuko ya saruji zaidi ya elfu kumi (10000) sambamba na mafuta ya kuweza kusukumia mitambo ya kufyatulia matofali.


 Amewaomba wananchi kushirikiana katika kuunga mkono jitihada hizo kwa kununua mifuko ya saruji.

Nae Kanali Charles Mbuge ambae ni Mwenyekiti  wa kamati ya ujenzi wa ofisi za walimu,ameelezea mafanikio waliyo yapata katika michango ya ujenzi huo ni milioni mia mbili ishirini na saba,  laki tatu ,ishirini  sita elfu na mia mbili.


Aidha ameelezea changamoto walizonazo ikiwamo ya kutoka katika baraza la mazingira NEMC kuhusu uchimbaji wa mchanga katika mto mpiji, upungufu wa mafuta wa mara kwa mara ,upungufu  wa malori unaosababisha kushindwa kufanya kazi nyakati za usiku ambapo kazi hizo hufanywa usiku na mchana ,upungufu wa vibao vya kufyatulia tofali ,ambapo idadi inayohitajika ni vibao elfu kumi, sambamba na ukosefu wa magari ya utawala.


"Mkuu wa Mkoa ametoa wazo la kusimamia maendeleo hayo kwa sababu anawapenda watanzania wote hasa wana Dar es salaam"Alisema Kanali  Charles.


Aidha amewasa wadau na wapenda maendeleo kuendelea kusaidia ili kutatua changamoto hizo na kufanikisha mradi huo wenye tija kubwa kwa Taifa.


No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages