Vyama vya
ushirika jijini Dar es salaam vimetakiwa kutumia ushirika huo kuanzisha viwanda vidogo ili kumuunga mkono
Rais wa jamhuri ya muuungano wa Tanzania
mhe. John Pombe Magufuli katika
ujenzi wa Tanzania ya viwanda na kukuza
uchumi wa wananchi na kutengeneza ajira kwa watanzania.
Mkuu
wa mkoa wa Dar essalaam mhe. Paul Makonda akitoa hotuba ya ufunguzi wa
mkutano Kauli hiyo
imetolewa na mkuu wa mkoa wa Dar es
salaam mhe. Paul Makonda wakati wa ufunguzi wa mkutano wa jukwaa la wana
ushirika mkoa wa Dar es salaam
uliofanyika Wilayani Kigamboni , na kuwasisitiza
wana ushirika hao kushiriki katka shughuli za maendeleo ya koa huo ikiwemo
kuchagia ujenzi wa ofis za walimu.
Aidha Makonda amwaetaka
wanaushirika hao kuzingatia sheria,
kanuni na tatatibu za kuanzishwa kwake ili kufikia malengo walojiwekea katika vyamahiyo.
Vilevile Miongoni mwa Changamoto
zilizotajwa kurudisha nyuma maendeleo ya
Ushirika ni pamoja na Makato makubwa ya
Fedha, Kucheleweshwa kwa Marejesho, Wakopaji kushindwa kulipa madeni na
kukimbilia kuweka zuio la kufilisiwa mali Mahakamani na Baadhi ya Waajiri
kutowasikisha makato na marejesho ya Wanachama waliokopa.
Hata hivyo
Kuhusu Changamoto hizo RC Makonda
amewataka Viongozi kuziandika Changamoto
hizo kisha kumpatia ili aziwasilishe kwenye ngazi husika ili ziweze kupatiwa
ufumbuzi.
Katika mkutano huo pia wanachama walipata
fursa ya kupiga kura na ku mchagua
mwenyekiti ,ambapo Tumain Wilfred alichaguliwa
na mara baada ya kucha guliwa ameeleza namna atakavyo itumika nafasi huku
akiweka wazi mabo yaliyolisababisha vyama vya ushika nchini kurudi nyuma kuwani udhaifu wa sheria ambapo sas imetungwa
sheria kali inayo weza kuwabana viongozi
wabadhirifu wa mali za ushirika .
Pamoja na
hayo wana ushirika wa mkoa huo wameiomba
serikali kupunguza tozo kwa vyama hivyo
ambavyo vina mtaji chini ya milioni 150 ili viweze kupiga hatua kimaendeeleo ,Mkoa wa Dar es salaam una jumla ya Vyama 763 vyenye wanachama zaidi ya 238,897.
No comments:
Post a Comment