Mtendaji Mkuu wa Mawasiliano na Masoko wa kampuni ya simu za
mkononi Tigo, William Mpinga (kushoto), akizungumza na waandishi wa habari
wakati wa kutangaza ofa kwa wateja watakao nunua tiketi za fista kwa tigopesa msimu mpya wa Tigo Fiesta 2017 'Tumekusoma (Kulia), ni Ofisa Biashara wa
tigo Edwin Mgoa hafla hiyo imefanyika leo jijini Dar es Salaam
Muda wa Maongezi, SMS na
Data za Bure kwa Wanunuzi wa Tiketi za ‘Tigo Fiesta 2017 - Tumekusomaa’
Tigo
inatoa dakika 100 za muda wa maongezi, SMS
100 SMS na and 100 Mbs za data kwa manunuzi yote ya tiketi kupitia TigoPesa
Dar es Salaam, Jumatatu
4 Septemba, 2017-
Huku ikiwa imebakia siku chache tu kabla ya onesho la kwanza la msimu wa Tigo Fiesta 2017 – Tumekusomaa
kufanyika jijini Arusha, wadhamini wakuu kampuni ya Tigo inazidi kutoa ofa
kabambe kwa wateja wote wa Tigo watakaonunua tiketi zao za awali kupitia huduma
ya TigoPesa.
Tigo
inatoa dakika 100 za bure, SMS 100 za bure, na
kifurushi cha 100Mbs cha data bure kwa wateja wote wa Tigo watakaonunua
tiketi zaoTigo Fiesta 2017 - Tumekusomaa kupitia huduma ya TigoPesa.
Akitangaza
ofa hiyo murwa jijini Dar es Salaam jana, Mkuu Mtendaji wa Huduma za Masoko wa
Tigo, William Mpinga alisema kuwa ofa hii mpya ya dakika 100 za muda wa
maongezi, SMS 100 na 100Mbs za data
inaenda sambamba na ofa iliyopo sasa ya punguzo ya bei asilimia 10% kwa tiketi
zote za awali za Tigo Fiesta 2017 zitakazonunuliwa kupitia Tigo Pesa au huduma
ya kuhamisha fedha ya mitandao mingine yote ya simu nchini.
‘Kama
tulivyoahidi hapo awali, tuna furaha kuthibitisha kuwa wateja wote wa Tigo
watakaonunua tiketi zao za ‘Tigo Fiesta 2017 Tumekusomaa’ kupitia Tigo Pesa,
moja kwa moja watapata bonasi ya dakika 100 za muda wa maongezi, SMS 100 na 100
Mbs za data bure kutoka Tigo. Hii ni pamoja na ofa nono ya punguzo la 10%
wanayopata wateja wote wa simu za mkononi wanaonunua tiketi zao za Tigo Fiesta
2017 kwa njia ya huduma ya kuhamisha fedha kwa njia ya mtandao wa simu.’
Aliongeza
kuwa ofa hii inaendana na sifa kuu ya Tigo kuwa mtandao unaowaelewa na kuwajali
zaidi wateja wake nchini.
Ili
kununua tiketi za Tigo Fiesta 2017 kwa njia ya mtandao na kupata ofa hizi
kabambe, mteja anahitaji kufuata hatua za kawaida za kutuma fedha na kutuma TZS
9,000/- kwenda namba 0678 888 888. Hapo mnunuzi atapokea ujumbe mfupi wa maneno
(SMS) utakathibitisha kuhusu manunuzi yake ya tiketi pamoja na ofa za dakika
100 muda wa maongezi, SMS 100 na 100Mbs za data kutoka Tigo.
‘Napenda
kuwaambia wateja wa Tigo wakae mkao wa kufaidika katika msimu huu wa Tigo
Fiesta 2017 kwa sababu kuna ofa nyingi za kusisimua ambazo tutazitanganza
katika siku zijazo,’ Mpinga alisema.
Mwaka huu msimu wa Tigo Fiesta 2017
– Tumekusomaa utajumuisha mikoa ya Arusha Kahama, Musoma, Mwanza, Tabora na
Dodoma. Tigo Fiesta 2017 – Tumekusomaa pia itatua katika mikoa ya Iringa,
Songea, Njombe, Sumbawanga, Morogoro, Tanga, Moshi na Mtwara, kabla ya
kuhitimishwa jijini Dar es Salaam.
No comments:
Post a Comment