Mstahiki Meya wa Manispaa ya Kinondoni Mh Benjamini
Sitta akizungumza na wanainchi wa
Manispaa hiyo katika uzinduzi rasmi wa zoezi la ulipaji fidia awamu ya kwanza
kwa wakazi 179 waliokamilisha utaratibu
wa malipo kwa walio athiriwa na mradi wa uboreshaji wa miundombinu ya barabara
mkoa wa Dar es Salaam. Katika uzinduzi huo mgeni rasmi alikuwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda
Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda ambae pia alikuwa mgeni rasmi akizungumza na wanainchi wa Manispaa ya Kinondoni katika uzinduzi rasmi wa zoezi la ulipaji fidia awamu ya kwanza kwa wakazi 179 waliokamilisha utaratibu wa malipo kwa
walio athiriwa na mradi wa uboreshaji wa miundombinu ya barabara mkoa wa Dar es
Salaam. Katika uzinduzi huo mgeni rasmi alikuwa Mkuu wa
Mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda
Baadhi ya wanainchi waliojitokeza katika uzinduzi huo
Mstahiki Meya wa Manispaa ya Kinondoni Mh Benjamini Sitta leo amezindua zoezi la *Ulipaji wa fidia* kwa Wakazi wanaopitiwa na *Mradi wa uboreshaji wa Barabara* kwa maeneo yasiyopangwa *DMDP* ambao wataanza kulipwa Fedha zao kuanzia *kesho* sambamba na kufanya ziara ya ukaguzi wa Miundombinu ya Barabara.
Mradi huo utahusisha uboreshaji wa *Barabara,Mabonde ya Mito, Ujenzi wa Mitaro ya Maji, Taa za Barabarani, Njia za watembea kwa Miguu, Vizimba vya taka, alama za Barabarani na Soko la Mwananyamala* ambapo unagharimu kiasi cha Shilingi *Billion 230*.
Miongoni mwa Barabara zitakazojengwa kwa kiwango cha lami ni Barabara inayoanzia *Morocco hotel hadi Sinza Kijiweni Km 5*, Barabara ya *Tandale Kisiwani kuelekea Mwananyamala* na Barabara za *Makumbusho, , TANESCO Msasani, Simu200, Kilungule na MMK.*
*Sitta* amesema mradi huo utafanya jiji la Dar es Salaam kuendelea kuwa la kisasa na kufikia azma yake ya Dar Mpya.
Amewataka wananchi watakaolipwa fidia kuhakikisha wanazitumia fedha hizo vizuri kwa kufungua miradi itakayowaingizia kipato.
Aidha *Sitta* amesema kuwa Kata za *Tandale, Mburahati na Mwananyamala* zitaingizwa kwenye idadi ya *Kata 14* zinazopandishwa viwango kwa kuwa Barabara za kisasa maana ya kuwa na *Lami,Taa na Mitaro ya Maji.*
Hata hivyo amesema *Mto Ng’ombe* pia utatengenezwa kwa kiwango cha kisasa urefu wa *Km 7.5* ili kuwezesha Maji kwenda moja kwa moja hadi Baharini kupitia eneo la Jangwani kutakapojengwa mfumo wa kusafirisha maji taka.
*Makonda* amempongeza Meya wa Kinondoni *Benjamin Sitta* na Manispaa hiyo na kuwataka kuhakikisha kila anaestahili kulipwa fidia analipwa kile anachostahili bila usumbufu.
No comments:
Post a Comment