Mkuu wa Wilaya ya Ilala Sophia Mjema amemtaka Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa hiyo kuwachukulia hatua wakandarasi wa magari ya taka ambao wamekuwa hawatimizi wajibu wao wa kuzoa taka.
Akizungumza leo jijini Dar es Salaam, kata ya Kiwalani DC Mjema alifikia hatua ya kutoa agizo hilo baada ya wakazi wa eneo hilo kulalamika kuwa wiki ya pili imepita mkandarasi anae husika na uzoaji taka eneo hilo kutokufanya kazi hiyo na kupelekea taka kuzagaa maeneo mbalimbali ya eneo hilo jambo ambalo ni hatari kwa afya.
" Watu wa namna hii Mkurugenzi inabidi wachukuliwe hatuaq kwa kukamatwa na kupelekwa mahakamani kwa kufanya mambo yaliyo nje ya makubaliano" Alieleza DC Mjema.
Pia DC Mjema amemuagiza Mkurugenzi huyo ndugu Msongela Palela kuhakikisha kuwa hakuna mradi wowote unafanyika katika kata husika bila ya ushirikishwaji wa wananchi ili baadae zisije kutokea sintofahamu na kwa pamoja wakubaliane bei za tozo za ada ya uzoaji taka katika maeneo hayo.
Katika hatua nyingine DC Mjema amewataka wananchi wa eneo hilo kwenda ofisi ya Mkurugenzi ili maeneo yao yapimwe kama yapo ndani ya hifadhi ya reli ili wajiandae mapema kabla ya bomoabomoa haijawafikia.
"Hili swala la bomoabomoa lipo nje ya uwezo wangu kwa wale wananchi ambao nyumba zao zipo kwenye hifadhi ya reli kati ya mita 30 na 50 waende ofisi ya Mkurugenzi kwa uhakiki" Alieleza DC Mjema.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Manispaa hiyo Palela amewataka watendaji wa mitaa kutowatoza wananchi tozo ya huduma wananchi pindi wanapokwenda katika ofisi zao, vinginevyo atawachukulia hatua, na kuwataka wananchi watoe taarifa kwa mtendaji wa kata, ikishindikana wakamuone yeye ofisini kwake.
No comments:
Post a Comment