A great place to access the latest news and information.

Breaking

Post Top Ad

Your Ad Spot

Tuesday, September 19, 2017

MASHINDANO YA KUMSAKA MR TANZANIA SASA KUONYESHWA MUBASHARA KWENYE RUNINGA

Tanzania bodybuilding federation imeandaa mashindano ya kumtafuta mr tanzania yani mr handsome na mr photogenic yatakayofanyika desemba 16 mwaka huuu jijini dar es salaam.

Akizungumza mbele ya waandishi wa habari jijini dar mwenyekiti wa mashindano hayo bwana nemes chiwalala  amesema mashindano hayo amabayo yamekuwa yakifanyika mara kadhaa kwa sasa yatafanyika mwezi desemba badala ya mwezi septemba kama ilivyopangwa hapo awali kutokana na washiriki kuomba kuongezewa muda zaidi kwa ajili ya kuendelea kufanya mazoezi.

" mshindi wa kwanza katika mashindano hayo atapata zawadi ya gari aina ya Noah pamoja na fedha taslimu milioni 10, mshindi wa pili atashinda kiasi cha milioni 5 huku mshindi wa tatu akipewa kitit cha shilingi milioni mbili na nusu" alisema Nemes.

Kwa upande wake bwana Nilesh Bhatt kutoka pilipili Entertainment ameongeza kuwa mashindano hayo yataweza kuonyeshwa mubashara katika kituo cha runinga cha Azam .

" washiriki waendelee kufanya mazoezi ili kuhakikisha wanajishindia zawadi nono ".

 Kwa upande wake   mohamed Orotu maarufu kama mzee Chilo amesema kama ilivyo kwa michezo mingine kuwa kama ajira kwa wachezaji hvyo watahakikisha mchezo huo wa kutunisha misuli unakuwa ni ajira pia kwa vijana wataoshiriki.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages