Commissioner in the Finance and Planning Ministry, John Rubaga (centre), Halotel Managing Director, Le Van Dai (left) and Finca Microfinance Bank Managing Director, Issa Ngwegwe applauses during the official launching of ‘Halo Yako’ service in Dart es Salaam yesterday. Halo Yako designed by Halotel and Finca will enable customers to save their money. Photo by Brian P
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
WIZARA YA FEDHA NA MIPANGO
HOTUBA YA WAZIRI WA
FEDHA, MHE. DKT. PHILIP ISDOR MPANGO (MB), WAZIRI WA FEDHA NA MIPANGO KATIKA
UZINDUZI WA HUDUMA YA HALO YAKO MALENGO INAYOENDESHWA KATI YA KAMPUNI YA
HALOTEL NA FINCA TANZANIA
SERENA HOTEL DAR ES
SALAAM,
5 SEPTEMBA , 2017
Ndugu Le Van Dai, Mkurugenzi wa Halotel Tanzania,
Ndugu Issa Ngwegwe, Mkurugenzi wa FINCA Tanzania,
Menejimenti na
Wafanyakazi wa Kampuni ya Halotel na
FINCA,
Wawakilishi wa Vyombo
vya Habari,
Wageni Waalikwa,
Mabibi na Mabwana.
Kwa
niaba ya Mheshimiwa Dkt. Philip Isdor Mpango, Waziri wa Fedha na Mipango,
napenda kuushukuru Uongozi wa Hallotel na FINCA kwa kumualika katika hafla hii
ya uzinduzi wa huduma mpya ya HALO YAKO ambayo nimeambiwa italeta faraja ya
kweli kwa wananchi, hususan wa kipato cha chini kwa kuwawezesha kujiwekea akiba
ili kufikia malengo yao kiuchumi na hali ya maisha kwa ujumla.
Hata
hivyo, kutokana na majukumu mengine ya Kitaifa aliyonayo, hususan katika
kipindi hiki cha vikao vya Bunge vilivyoanza leo hii Dodoma, Mhe. Waziri ameshindwa
kuhudhuria katika tukio hili muhimu na hivyo amenituma nimwakilishe. Ninamshukuru
sana kwa dhamana hiyo na natumaini kwamba nitaifanya kazi hiyo ipasavyo.
Wageni
waalikwa, Mabibi na Mabwana, Serikali inatambua kwamba jitihada za Kukuza
Uchumi na Kupunguza Umaskini haziwezi kuwa na mafanikio bila kushirikisha Sekta
Binafsi, hususan Makampuni ya Mawasiliano ya simu.
Vilevile, Serikali imekuwa ikifanya mageuzi
mbalimbali kwa mtazamo wa kuiwezesha Sekta Binafsi kuwa Injini ya Ukuaji wa
Uchumi wetu, ambapo tangu kuingia kwa Mfumo wa Soko Huria hapa Nchini, Sekta
Binafsi imeweza kuchukua nafasi yake na kuwekeza katika huduma mbalimbali
zikiwemo huduma za simu hususan huduma za kifedha kwa njia ya simu za mkononi.
Sisi
kama Serikali tutaendelea kuhakikisha kuwa uhusiano wa karibu uliopo kati ya
Serikali na Sekta Binafsi zikiwemo Kampuni za mawasiliano ya simu unadumishwa.
Aidha, tutaendelea kuheshimu mchango wa Sekta Binafsi ambao ni kichocheo
kikubwa kwa Uchumi na maendeleo ya Taifa letu.
Vilevile, Serikali itaendelea na jukumu lake la kuboresha mazingira ya
uwekezaji ili kuhamasisha wawekezaji zaidi Nchini.
Ndugu Wageni Waalikwa, ninaitambua
Halotel Tanzania kuwa ni miongoni mwa kampuni za simu hapa Tanzania zinazoongoza
kwa kutoa huduma za kibunifu za mawasiliano zenye wigo mpana na kuchangia
katika shughuli mbalimbali za maendeleo na Taifa kwa ujumla; hali kadhalika,
FINCA kwa kutoa huduma mbalimbali za kibenki kwa watanzania wengi mijini
na vijijini. Kwa niaba ya Mheshimiwa
Waziri wa Fedha na Mipango, ninaomba mniruhusu nichukue fursa hii kuwapongeza
Halotel Tanzania na FINCA kwa jitihada zao za kuiunga mkono Serikali
yetu katika kutoa huduma za mawasiliano, kifedha na kuongeza ajira ndani ya
jamii yetu.
Ndugu Wageni Waalikwa, huduma za kifedha kwa njia ya simu
za mkononi zimekuwa ni muhimu na kichocheo kikubwa katika maendeleo ya
nchi yetu. Serikali tunaunga mkono jitihada hizi kwani zinaleta mapinduzi na
maendeleo huku zikichangia kubadili maisha ya watanzania wengi na kuwawezesha
kuwa na mifumo rasmi ya kutuma na kupokea pesa. Maendeleo ya kiuchumi
yamechochea watanzania wengi kutumia simu zao za mkononi kwa kufanya miamala
mbalimbali ya kifedha katika akaunti zao mahali popote walipo.
Asanteni sana Halotel kwa kufika kila kona ya
Nchi yetu, hivyo kurahisisha upatikanaji wa huduma hizi.
Niwapongeze tena Halotel na FINCA
kwa kuingia katika ushirikiano huu; ninaona faraja kubwa sana kutambua kuwa
sekta ya fedha inaendelea kupata mdau mwingine katika kuhakikisha huduma za
fedha zinasambaa kote nchi nzima.
Mabibi
na Mabwana, wengi wetu kama sio wote hapa tunatumia huduma za simu katika
kutuma na kupokea fedha na hata kujiwekea akiba, pengine mniruhusu kwa uchache
tu kuizungumzia huduma ya HALOPESA. Nimeelezwa kuwa, huduma hii ya HALOPESA
tangu ilipoanzishwa imeleta mapinduzi makubwa, jinsi tunavyotuma na kupokea
pesa kwa ndugu jamaa na marafiki popote pale nchini kwa urahisi, uharaka na kwa
usalama zaidi.
Huduma hii imekuwa mkombozi mkubwa kwa
wajasiliamali wengi na wananchi wanaoishi vijijini. Niipongeze tena kampuni ya
HALOTEL pamoja na kampuni zingine kwa kazi hii kubwa mnayoifanya kuhakikisha
huduma ya fedha kupitia mitandao ya simu inabakia kuwa ya uhakika na ya
kuaminika; na pia kwa namna mnavyoshirikiana na wadau mbalimbali kuhakikisha
kwamba kuna mafanikio makubwa sokoni ambayo kwayo yanaleta tija kwa wananchi
wetu.
Aidha, nitoe wito kwa makampuni yote ya simu
kuendelea kutoa huduma zenye gharama nafuu kwa wananchi na kwa uwazi zaidi.
Mkumbuke kuwa mamilioni ya wananchi wanawaamini na kuthamini ubora wa bidhaa na
huduma zenu.
Mabibi na Mabwana, napenda kuwaasa kidogo
Kampuni ya HALOTEL kwamba, japo mmekuwa wabunifu katika huduma za mawasiliano,
msibweteke! Bali sasa ni muda muafaka wa kuendelea kuongeza juhudi katika mambo
yafutayo:
·
Endeleeni kuwa wabunifu zaidi na kuboresha huduma kwa wateja ili Kampuni iweze kupata
faida kubwa zaidi na hivyo kulipa kodi kubwa kwa Serikali na kuchangia
maendeleo ya Taifa;
·
Endeleeni kutimiza wajibu wenu ili huduma
mnazozitoa ziweze kuwafikia wananchi wengi zaidi na kwa gharama nafuu; na
·
Endeleeni kuhamasisha wananchi wajiunge na huduma hii mpya ya HALO YAKO na wasaidieni
wananchi wa kipato cha chini kufikia
malengo yao na hatimaye waweze kuongeza kipato chao na cha taifa kwa ujumla.
Kwa niaba ya Waziri
wa Fedha na Mipango, nimalizie kwa kuwashukuru nyote mliofika hapa kushuhudia
uzinduzi huu. Nina imani kwamba kwa pamoja sote tutakuwa mabalozi wazuri wa
huduma hii ya HALO YAKO. Wito
wangu kwa Wananchi wote ni kwamba, tumieni kikamilifu huduma hii mpya ya HALO
YAKO inayozinduliwa leo ili muweze
kuendeleza shughuli zenu za maendeleo. Mwisho kabisa, nawatakia
Halotel na FINCA ufanisi zaidi katika shughuli zenu za kila siku ili kwa pamoja
tusaidiane kujenga Taifa letu.
Wageni
waalikwa, Mabibi na Mabwana, kabla sijahitimisha hotuba hii, naomba niyaseme
machache kwa lugha ya kigeni kwa manufaa ya wale ambao hawajabahatika kuijuwa
lugha hii adhimu ya Kiswahili:
Ladies
and Gentlemen:
Allow
me to share with you few messages in English for the benefit of some of us:Let me express my sincere gratitude
for the honor accorded to the Minister for Finance and planning, Hon.
Philip I. Mpango (MP) at this auspicious occasion of launching HALO YAKO
Service by Halotel and Finca. I am really humbled and privileged to
represent him, since he could not make it due to other pressing public
service responsibilities, particularly at the time when Parliamentary
Sessions start today. Kindly accept his apology. I trust I will be able to
represent him well.
The role of the financial sector is
to transfer funds from surplus units to deficit units, thereby promoting
greater efficiency and economic growth by channeling funds from people who
do not have productive use for them to those who do.
This includes among
others, mobilizing savings from the population, guarding against uncertainty,
assessing risks and providing credit.
Along these lines, the financial sector finds itself capable of linking
economic agents in the manner that supports expansion of economic
opportunities, creates jobs, and generates revenue for the Government
. This is
what Halotel and Finca Tanzania are trying to achieve!On behalf of Hon. Minister, may I
take this opportunity to congratulate them for joining forces to create a
service such as this one which we are about to launch today; the service is
geared towards assisting millions of Tanzanians, who may have no easy
access to conventional banking facilities; indeed this is financial inclusion
at work
!One of the biggest challenges we
face today is the ability to mobilize savings and access to credit at
affordable prices. However, there is enough evidence to show that
technology can significantly help to reduce some of the barriers to access,
such as remoteness and cost of providing financial services.
It is our
sincere hope that, the product we are about to launch today will meet our
expectations on what technology can facilitate to achieve!Finally, while efforts need to be sustained
to further increase inclusion and access, there is a need to expand and
sustain digital financial services ecosystem, including money transfer
platforms, payment solutions, savings, financing, micro-insurance,
financial planning and access to capital markets securities.
I trust that
Halotel and Finca Tanzania, and indeed all stakeholders in the financial
system will continue to be innovative in designing various products that
can cater for long-term needs of customers at affordable prices.The Government recognizes the role
of the private sector in Tanzania’s economic growth endeavours, and will
therefore continue to support it.
Wageni waalikwa, Mabibi na Mabwana, baada ya kusema hayo,
sasa napenda kutamka kwamba niko tayari Kuzindua rasmi huduma ya HALO YAKO inayomwezesha
hasa mwananchi wa kipato cha chini kuweza kujiwekea akiba na kufikia malengo
yake.
Asanteni
sana kwa kunisikiliza.
No comments:
Post a Comment