Kikosi
cha Polisi cha Usalama Barabarani kimesema kuwa ajali za barabarani
zinaweza kupungua kwa madereva kufuata sheria za usalama barabarani.
Hayo
ameyasema Kamanda wa Polisi wa Kikosi cha Usalama Barabarani
kamishina msaidizi mwandamizi wa jeshi la polisi(SACP) Fortunatus
Musilim wakati akizindua uwekaji wa namba maalum za simu katika mabasi
yaendayo mikoani na nchi jirani leo katika kituo cha Ubungo jijini Dar
es Salaam.
Amesema
kuwa namba za simu katika mabasi hayo zitatumika kwa abiria kutoa
taarifa ya dereva anaendesha bila kufuata sheria za usalama barabarani
ikiwemo mwendo kasi.Kamanda
Muslim amesema kuwa namba hizo ni bure na kwa abiria, dereva au
kondakta atakaeng’oa namba hizo atachukuliwa hatua ikiwemo kunyanganywa
leseni.
Amesema
uwekaji wa namba maalumu kwenye mabasi unafanyika nchi nzima ikiwa yote
nikulinda maisha ya abiria katika kuwa na uhakika wa safari zao.
Kamanda
wa Polisi wa Kikosi cha Usalama Mkoa wa Kinondoni, Solomon Mwangamilo
amesema kuwa watasimamia maagizo ya Mkuu wa Jeshi la Polisi (IGP), Simon
Sirro ambapo yamekaziwa na Kamanda wa Polisi wa Kikosi cha Usalama
Barabarani kamishina msaidizi mwandamizi wa jeshi la polisi(SACP)
Fortunatus Musilim.
Mkuu
wa Usalama Barabarani Kituo cha Ubungo Ibrahim Samwix amesema kuwa kila
siku wanafanya ukaguzi na gari ambayo ina kasoro haiwezi kufanya safari
zake.Amesema watahakikisha kuwa kila basi linalondoka katika kituo cha ubungo linakuwa na namba maalum za simu katika kila basi..
Kamanda
wa Polisi wa Kikosi cha Usalama Barabarani kamishina msaidizi
mwandamizi wa jeshi la polisi(SACP) Fortunatus Musilim akizungumza na
waandishi habari katika uzinduzi wa uwekaji wa namba maalum za simu
katika mabasi yaendayo Mikoani na Nchi jirani katika kituo Kikuu Cha
Mabasi Ubungo jijini Dar es Salaam.
Kamanda
wa Polisi wa Kikosi cha Usalama Barabarani Mkoa wa Kinondoni, Solomon
Mwangamilo akizungumza na waandishi wa habari kuhusu mkazo na maagizo ya
Ukaguzi wa magari katika kituo Kikuu Cha Mabasi Ubungo jijini Dar es
Salaam.
Mkuu
wa Usalama Barabarani Kituo cha Ubungo Ibrahim Samwix (katikati)
akizungumza na waandishi habari kuhusu ukaguzi magari yanayotoka kituo
Kikuu Cha Mabasi Ubungo jijini Dar es Salaam.
Kamanda
wa Polisi wa Kikosi cha Usalama Barabarani kamishina msaidizi
mwandamizi wa jeshi la polisi(SACP) Fortunatus Musilim akiweka namba
maalmu za simu katika basi itakayotumika kupiga kwa abiria kwa dereva
atakaye kiuka sheria za usalama barabani .
Askari wa Usalama barabani wakiwa katika ukaguzi mbalimbali wa mabasi katika kituo Kikuu cha Mabasi Ubungo.
Muonekano wa Mabasi yakiwa katika kituo Kikuu cha Ubungo leo asubuhi
No comments:
Post a Comment