MWENYEKITI
wa Taasisi ya sekta binafsi nchini (TPSF) Dr. Reginald Mengi amezitaka
Nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki kushirikiana katika kutumia utajiri
wake mkubwa wa raslimali kunufaika kiuchumi. Ushirikiano huo ni pamoja
na kuzindeleza raslimali hizo na kutumia nembo moja ya kibiashara ili
kuzalisha mabilionea wakubwa duniani.
Mwenyekiti
huyo alisema hayo katika mkutano wa Taasisi za Sekta Binafsi za
Tanzania na Kenya zilizokutana jijini Dar es salaam kujadili kwa pamoja
namna ya kuondoa vikwazo vya kufanya biashara baina ya wafanyabiashara
wa nchi hizo mbili. Mwenyekiti
wa Taasisi ya sekta binafsi nchini (TPSF) Dr. Reginald Mengi
akizungumza wakati akifungua mkutano wa Taasisi za Sekta Binafsi za
Tanzania na Kenya zilizokutana jijini Dar es salaam kujadili kwa pamoja
namna ya kuondoa vikwazo vya kufanya biashara baina ya wafanyabiashara
wa nchi hizo mbili uliofanyika jijini Dar es Salaam.
Pamoja
na kutoa wito huo Dk Mengi pia amempongeza Rais wa Tanzania Dk John
Pombe Magufuli pamoja na serikali yake kwa kuwa mstari wa mbele
kuboresha ushirikiano wa kiuchumi kati ya Tanzania na Kenya. Aidha
alisema dhamira yake ya kuigeuza Tanzania kuwa nchi ya viwanda itasaidia
kuwakwamua Watanzania kutoka katika umaskini. Katika mazungumzo hayo
ujumbe wa Tanzania uliongozwa na Mwenyekiti wa Taasisi ya Sekta Binafsi
Tanzania –TPSF Dr Reginald Mengi na Ujumbe wa Kenya umeongozwa na Gavana
wa Taasisi ya Sekta Binafsi ya Kenya – KEPSA Bw. George Owuor. Gavana
wa Taasisi ya Sekta Binafsi ya Kenya – KEPSA Bw. George Owuor
akimpongeza Mwenyekiti wa Taasisi ya sekta binafsi nchini (TPSF) Dr.
Reginald Mengi kwa kutoa risala nzuri ya ufunguzi wa mkutano huo.
Akizungumza
katika mkutano huo Mkurugenzi Mtendaji wa TPSF Bw. Godfrey Simbeye
amesema mkutano huo umeitishwa kutokana na kujitokeza vikwazo vya
kufanya biashara baina ya Wafanyabiashara wa Tanzania na Kenya, jambo
linalokwamisha malengo ya Jumuiya ya Afrika Mashariki ya kujenga uchumi
unaoongozwa na sekta Binafsi. Kwa upande wake Kiongozi wa Ujumbe wa
KEPSA Bw. George Owuor amesema Wafanyabiashara wa Kenya wanapenda sana
kushirikiana kibiashara na wenzao wa Tanzania, na wangependa kuona
vikwazo vinavyokwamisha mahusiano ya kibiashara vinaondolewa. Gavana
wa Taasisi ya Sekta Binafsi ya Kenya – KEPSA Bw. George Owuor
akiwasilisha mada kuhusu kupunguza pengo la biashara kati ya Tanzania na
Kenya na kutumia fursa zilizopo na kutanua biashara nje ya mipaka
katika mkutano wa Taasisi za Sekta Binafsi za Tanzania na Kenya
zilizokutana jijini Dar es salaam kujadili kwa pamoja namna ya kuondoa
vikwazo vya kufanya biashara baina ya wafanyabiashara wa nchi hizo mbili
uliofanyika jijini Dar es Salaam. Meneja
anayeshughulikia Utafiti, Uchambuzi na Sera wa Taasisi ya Sekta Binafsi
ya Kenya – KEPSA, Victor Ogalo (kushoto) akitoa mada kuhusu changamoto
za kisera za Tanzania na Kenya katika mkutano huo uliofanyika jijini Dar
es Salaam. Kulia walioketi ni Gavana wa Taasisi ya Sekta Binafsi ya
Kenya – KEPSA Bw. George Owuor na Mwenyekiti wa Taasisi ya sekta binafsi
nchini (TPSF) Dr. Reginald Mengi wakifuatilia kwa umakini mada hiyo. Mkurugenzi
Mtendaji wa TPSF Bw. Godfrey Simbeye (kulia) na Mkurugenzi Mtendaji wa
kampuni ya Alaska Tanzania, Jennifer Bash wakifuatilia mada mbalimbali
zikizokuwa zikiwasilishwa ukumbini hapo katika mkutano wa Taasisi za
Sekta Binafsi za Tanzania na Kenya zilizokutana jijini Dar es salaam
kujadili kwa pamoja namna ya kuondoa vikwazo vya kufanya biashara baina
ya wafanyabiashara wa nchi hizo mbili uliofanyika jijini Dar es Salaam. Pichani
juu na chini ujumbe wa Tanzania na Kenya ulioshiriki mkutano wa Taasisi
za Sekta Binafsi za Tanzania na Kenya zilizokutana jijini Dar es salaam
kujadili kwa pamoja namna ya kuondoa vikwazo vya kufanya biashara baina
ya wafanyabiashara wa nchi hizo mbili uliofanyika jijini Dar es Salaam. Gavana
wa Taasisi ya Sekta Binafsi ya Kenya – KEPSA Bw. George Owuor na
mwenyeji wake Mwenyekiti wa Taasisi ya sekta binafsi nchini (TPSF) Dr.
Reginald Mengi katika mkutano huo. Mkurugenzi
Mtendaji wa TPSF Bw. Godfrey Simbeye akijibu maswali kwa waandishi wa
habari (hawapo pichani). Kulia ni Mwenyekiti wa Taasisi ya sekta binafsi
nchini (TPSF) Dr. Reginald Mengi.
No comments:
Post a Comment