Benki Kuu ya Tanzania imetoa leseni kwa kampuni mpya ya kutoa mikopo ya nyumba inayoitwa “First Housing Company (Tanzania) Limited”.
Taarifa iliyotolewa na Idara ya Sera na Leseni katika Kurugenzi ya Usimamizi wa Mabenki imeeleza kwamba leseni hiyo inaipa nafasi kampuni hiyo mpya kufanya biashara ya kutoa mikopo ya nyumba nchini. Makao makuu ya kampuni hiyo ni jijini Dar es Salaam.
Hii ni mara ya kwanza kwa Benki Kuu kutoa leseni kwa kampuni ya mikopo ya nyumba nchini.
Benki Kuu pia inatoa leseni na kusimamia benki, taasisi za fedha, maduka ya kubadilisha fedha, kampuni za karadha na zinazotunza kumbukumbu za ukopaji za wananchi (credit reference bureaus).
No comments:
Post a Comment