A great place to access the latest news and information.

Breaking

Post Top Ad

Your Ad Spot

Monday, July 17, 2017

Wafanyakazi wa Cartrack Tanzania wajitolea kupanda miti ya matunda na mboga Kituo cha Watoto cha Malaika, Mkuranga, Pwani

Mkurugenzi Mtendaji kampuni ya utengenezaji na uwekaji wa vifaa vya kuratibu matumizi ya magari na kusaidia upatinakaji wa magari yaliyoibiwa ya Cartrack Tanzania, Bi. Anna Nyimbo (mwenye jembe), akipiga tuta la kupandia mbogamboga katika eneo la kijiji cha watoto yatima cha Malaika, katika hafla ambayo wafanyakazi wa kampuni hiyo walipanda miti ya matunda na mbogamboga na kisha kukabidhi msaada wa aina mbalimbali za vyakula ikiwa ni sehemu ya shughuli za kijamii kwa kituo hicho kilichopo Mkuranga mkoani Pwani jumamosi iliyopita.
Meneja Uendeshaji wa kampuni ya utengenezaji na uwekaji wa vifaa vya kuratibu matumizi ya magari na kusaidia upatinakaji wa magari yaliyoibiwa ya Cartrack Tanzania, Bi. Jayne Nyimbo (katikati), akipanda miti pamoja na baadhi ya watoto wanaolelewa katika kituo cha watoto yatima cha Malaika Village, katika hafla ambayo wafanyakazi wa kampuni hiyo walipanda miti ya matunda na mboga mboga na kisha kukabidhi msaada wa aina mbalimbali za vyakula ikiwa ni sehemu ya shughuli za kijamii kwa kituo hicho kilichopo Mkuranga mkoani Pwani.
Mkurugenzi Mtendaji kampuni ya utengenezaji na uwekaji wa vifaa vya kuratibu matumizi ya magari na kusaidia upatinakaji wa magari yaliyoibiwa ya Cartrack Tanzania, Bi. Anna Nyimbo (kulia), akikabidhi msaada wa aina mbalimbali za vyakula kwa Meneja wa kijiji cha Malaika, James Kalinga (kushoto), katika hafla hiyo. 
Baadhi ya wafanykazi wa Kampuni ya Cartrack wakisaidia kuandaa shamba kwa ajili ya upandaji wa mbogamboga katika hafla hiyo.
Mmoja wa wafanyakazi wa Kampuni ya Cartrack, Albert Mdemu (katikati), akipanda miti pamoja na watoto wanaolelewa katika Kijiji cha watoto yatima cha  Malaika, kilichopo Mkuranga, Pwani juzi.
Baadhi ya wafanyakazi wa Kampuni ya Cartrack wakisaidia kuandaa shamba kabla hawajapanda mbogamboga ikiwa ni sehemu ya shughuli za kusaidia jamii.
Watoto wanaolelewa katika Kijiji cha Malaika wakifurahi pamoja na wafanyakazi wa Cartrack waliotembelea katika makazi yao na kuwasaidia katika upandaji miti ya matunda na mbogamboga.
Watoto wanaolelewa katika Kijiji cha Malaika wakila chakula huku wakimsikiliza Mkurugenzi Mtendaji wa Cartrack Tanzania, Anna Nyimbo (kulia nyuma), walipowatembelea katika makazi yao na kuwasaidia katika upandaji miti ya matunda na mbogamboga.
Meneja Uendeshaji wa Cartrack Tanzania, Bi. Jayne Nyimbo (katikati) akiwa na baadhi ya watoto wanaolelewa katika Kijiji cha Malaika.
Watoto wanaolelewa katika Kijiji cha Malaika wakiwasindikiza baadhi ya wafanyakazi wa Cartrack baada ya kuhitimisha ziara yao kituoni hapo. Mkurugenzi Mtendaji wa Cartrack, Bi. Anna Nyimbo alisema miti ya matunda na mbogamboga walizopanda zitawasaidia watoto hao katika mahitaji  ya kila siku hivyo kupunguza utegemezi wa misadaa. (All photo vby Peter Mgongo)

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages