Meneja
Malezi wa Taasisi ya Ujasiriamali na Ushindani Tanzania (TECC), Bw.
Daniel Mghwira (katikati) akizungumza kuhusu kuanza kwa kwa awamu ya
tatu ya program Via Jiandalie Ajira kwa halmashauri zote za Dar es
Salaam, Mkindani Mtwara, Dodoma na Kibaha Pwani, kulia ni Mkurugenzi
Mtendaji wa Mfuko wa Rais wa Kujitegemea (PTF),Bi. Haigath Kitala na
kushoto Mwakilishi wa Mkurugenzi Mtendaji wa Chemba ya Wafanyabiashara
na Kilimo Tanzania(TCCIA),Bi. Magdalene Mkocha.
Vijana
wenye umri wa miaka 18 hadi 24 wameshauriwa kujiunga na awamu ya tatu
ya program Via Jiandalie Ajira inayoendeshwa na Taasisi ya Ujasiriamali
na Ushindani Tanzania (TECC) ili kupata mafunzo ya ujasiriamali, stadi
za maisha, malezi ya kibiashara na kuunganishwa na taasisi za kifedha
kupata mitaji kukabiliana na tatizo la ajira.
Meneja
Malezi wa Taasisi hiyo, Bw. Daniel Mghwira alisema hayo jijini Dar es
Salaam wakati akizungumza na waandishi wa habari, kuwa vijana wajiunge
na program hiyo ambayo imeingia katika awamu ya tatu kupata mafunzo hayo
ili kukabiliana na tatizo la ajira.
“Via
Jiandalie Ajira awamu ya tatu inawalenga vijana wa Halmashauri zote za
Mkoa wa Dar es Salaam, Mikindani Mtwara, Dodoma na Kibaha Pwani,” na
fomu za kujiunga zinapatikana katika ofisi za kata, ofisi za maafisa
vijana za manispaa za maeneo hayo, aliongeza kusema Bw. Mghwira ambaye
pia ni Naibu Mkurugenzi wa taasisi hiyo.
Pia
fomu hizo zinapatikana katika ofisi za Shirika la Kuhudumia Viwanda
Vidogovidogo (SIDO) na Chemba ya Wafanyabiashara na Kilimo Tanzania
(TCCIA).
Alifafanua
kwamba fomu hizo zinatolewa bila ya gharama ambapo vijana watakao
chaguliwa watafundisha mafunzo ya ujasiriamali, stadi za maisha, malezi
ya kibiashara na kuwaunganisha na taasisi za kifedha kupata mitaji kwa
njia ya mikopo kwa masharti nafuu, hivyo ni fursa kwa vijana wa maeneo
hayo.
Alisema
kuanzia sasa hadi mwaka 2020 taasisi yao kupitia program hiyo
itafundisha vijana ,3,000 katika mikoa hiyo na hiyo itafanya jumla ya
vijana 4,000 wakijumlishwa na waliofundishwa katika program ya kijana
jiajiri.
Mkurugenzi
Mtendaji wa Mfuko wa Rais wa Kujitegemea (PTF),Bi. Haigath Kitala
alisema serikali imetoa kipaumbele katika uchumi wa viwanda, vijana
wanahitajika kutumia fursa hiyo ili wasije kuwa watazamaji katika uchumi
huo.
“Vijana
wanapokuwa wamepata mafunzo kama haya, ni rahisi kwa mfuko wao
kuwapatia mikopo ya riba nafuu,” na mfuko huo unatoa mikopo kwa vijana
waliohitimu mafunzo ya ufundi stadi na wanawake wazalishaji mali na
wanahitajika kuwa katika vikundi, alisema.
Alisema pia mfuko unatoa mkopo wa vifaa na wa dhabuni sababu vijana wengi wanashindwa kutekeleza dhabuni hizo kwa kukosa fedha.
Mwakilishi
wa Mkurugenzi Mtendaji wa Chemba ya Wafanyabiashara na Kilimo
Tanzania,Bi. Magdalene Mkocha alisema chemba inashirikiana na taasisi
hiyo katika kuwaandaa vijana kuingia katika ujasiriamali husani katika
kutoa malezi.
“Tunapotaka
kujenga kada nzuri ya wajasiriamali ni lazima kwa pamoja tushiriki
katika hili,” na alitoa ombi kwa serikali na wadau wote kusaidia
kusukuma jambo hilo,alisema.
Naye
kijana ambaye amenufaika na mafunzo ya taasisi hiyo, Jackson Mmbando
alisema mafunzo yanayotolewa na TECC yamewezesha kuanza na kuendesha
biashara yake kwa mafanikio makubwa na anawataka vijana wenzake kuwa na
nidhamu ya fedha ili kuanza au kuendeleza biashara.
Program
hiyo ya Via Jiandalie Ajira inatekelezwa na TECC kwa kushirikiana na
wadau wake kama Taasisi ya Kuendeleza Vijana Kibiashara ya Marekani
(IYF), Mfukoa wa Rais wa Kujitegemea (PTF), SIDO, TCCIA , Manispaa au
Halamashauri za Miji na Wilaya na sasa imefikia awamu ya mwisho kwa
mwaka 2017.
No comments:
Post a Comment