Naibu
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais (TAMISEMI), Mhe. Selemani Jafo akikabidhiwa
fomu ya kujiunga na Mfuko wa Pensheni wa PSPF kupitia Mpango wa
uchangiaji wa Hiari, (PSS), kutoka kwa Mfkurugenzi wa Uendeshaji, Bi.
Neema Muro, (kulia), baada ya kufungua semina ya Mafunzo kwa wastaafu
watarajiwa mkoni Dodoma Julai 14, 2017.
Na Yusuph Mlandula
NAIBU
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Tamisemi, Mhe. Selemani Jafo amejiunga na
Mfuko wa Pensheni wa PSPF kupitia Mpango wa uchangiaji wa Hiari, (PSS)
na kuhimiza na kjtoa wito kwa waajiri wote nchini kuwasilisha michango
ya wafanyakazi wao katika mifuko ya hifadhi ya jamii kwa wakati kama
sheria inavyowataka ili kuepuka usumbufu kwa wanachama wakati wa kupata
Mafao yao wanapostaafu.
Mhe.
Jafo aliyasema hayo wakati akifungua semina ya mafunzo kwa wastaafu
watarajiwa mkoani Dodoma Julai 14, 2017.Semina hiyo imelenga kuwajengea
uwezo wastaafu hao watajiwa ili kuweza kufanya shughuli za ujasiriamali
wakati muda wao wa utumishi wa umma utakapokoma.
Mhe.
Jafo amewanyooshe kidole waajiri wenye tabia ya kutopeleka michango ya
wanachama katika mifuko yao kitendo ambacho kinasababisha kero kubwa
pindi watumishi hao wanapostaafu na kuanza kuhangaikia Mafao yao
kutokana na taarifa za uwasilishaji michango katika Mifuko ya Hifadhi ya
Jamii kutokamilika.
“Nitoe
rai kwa ndugu zangu watumishi wa umma ambao katika kipindi cha miaka
miwili ijayo mtaondoka kwenye utumishi wa umma, yatumieni vema mafunzo
haya ili mtakapopata mafao yenu basi tayari mtakuwa na nyenzo ya
kuwasaidia kutumia vema fedha mtakazopata kwa kuanzisha viwanda vidogo
vidogo, lakini pia kilimo na ufugaji wa kisasa na hatimaye kuyafanya
maisha yenu kuwa bora baada ya utumishi wa umma.” Aiasa Mhe. Jafo.
Katika
hatua nyingine, wimbi la viongozi kujiunga na Mpango wa uchangiaji wa
Hiari yaani PSPF Supplementary Scheme, (PSS), Mhe. Jafo naye amejiunga
na mpango huo na kuwahamasisha wastaafu hao watarajiwa na wananchi
wengine kujiunga na Mpango huo kwani utawawezesha kuwa na hakikisho la
kuweka fedha zao ili ziwasaidie kwenye miradi wanayotarajia kuibuni,
ikiwa ni pamoja na kujipatia bima ya afya.
Kwa
upande wake Mkurugenzi Mkuu wa PSPF Bw. Adam Mayingu, amebainisha kuwa
mfuko huo unatarajia kulipa jumla ya Sh.Trilioni 1.3 katika kipindi cha
2017/18 ambazo ni Mafao ya watumishi 9,552 wanaojiandaa kustaafu katika
kipindi cha kati ya Mwaka huu wa 2017 na mwaka ujao wa 2018.
No comments:
Post a Comment