WAZIRI
wa Fedha na Mipango, Mhe Dkt. Philip Mpango ametaka kuwapo na uratibu
wenye maslahi mapana katika biashara na uwekezaji kati ya Tanzania na
China.
Alisema
hayo wakati akifungua mkutano wa 6 wa mwaka wa ESRF unaozungumzia
biashara na uwekezaji kati ya Tanzania na China.
Alisema mahusiano yaliyopo kati ya Tanzania na China ambayo ni ya
kihistoria yasitumike vibaya bali yanahitaji kuratibiwa kiuangalifu kwa
maslahi ya pande zote mbili.
Aliwataka
washiriki wa mkutano huo wa mwaka kujadili kwa makini namna ya kuratibu
vizuri vitega uchumi na biashara kwa manufaa ya nchi zote mbili.
Alielezea
kufurahishwa kuwapo na mada mbalimbali zinaozungumzia biashara na
uwekezaji kati ya Tanzania na China na kusema mada hizo zitumike vyema
kuweka misingi mizuri yenye manufaa kwa pande zote mbili. Aidha
aliipongeza ESRF kwa kuona haja ya kuwapo kwa mazungumzo ya aina hiyo na
kusema kupitia tafiti mbalimbali taifa hili litaenda mbele katika
kujenga uchumi wa viwanda.
Mkutano huo unaohusisha washiriki mbalimbali wa ngazi za juu wa biashara
na uwekezaji kati ya Tanzania na China umeitwa kama sehemu ya mchango
wa ESRF katika ujenzi wa uchumi wa viwanda wa Tanzania. “Sisi serikalini
tunaridhishwa na juhudi zinazofanywa na taasisi za kitafiti kama hii
zenye lengo la kusaidia juhudi za serikali za kuhudumia watu wake na
kuongeza ustawi” alisema Mpango.
Mkutano
huo ambao unazungumzia mahusiano ya kibiashara na uwekezaji umeelezwa
na Mh. Dk Mpango kuwa moja ya mikutano inayotoa fursa za kuangalia
uwekezaji wenye tija unaozingatia maslahi mapana ya mataifa husika.
Alisema
Tanzania na China zina uhusiano mzuri wa kihistoria na hadi sasa na
kwamba kinachostahili ni kuoanisha uhusiano huo na kuuweka katika hali
bora zaidi za kunufaisha pande zote mbili.
Baadhi
ya miradi mikubwa ambayo Tanzania imesaidiwa na China ni pamoja na
ujenzi wa Reli ya Tanzania na Zambia (TAZARA) na kiwanda cha Urafiki;
kuanzishwa kwa shamba la mpunga la Mbarali; kiwanda cha sukari cha
Mahonda na mgodi wa mawe wa Kiwira.
Kwa
sasa China ni moja ya taifa lililo na uwekezaji mkubwa nchini Tanzania
pia ikifanya shughuli nyingi za ujenzi zenye gharama kubwa kama daraja
la Kigamboni na barabara.
Naye
Mwenyekiti wa bodi ya ESRF, Philemon Luhanjo, akimkaribisha Mheshimiwa
Waziri Mpango alisema kwamba alisema kwamba mkutano huo umeandaliwa kwa
pamoja kati ya ESRF na Chuo kikuu cha Kilimo cha China. Alisema mkutano
huo umewaleta pamoja wanazuoni wa Kichina na Kitanzania kuangalia
mahusiano yaliyopo na kutengeneza mustakabli bora wa namna ya
kushirikiana.
Naye
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Tafiti za Kiuchumi na Kijamii (ESRF),
Dk. Tausi Kida amesema kwamba mkutano huo ni sehemu ya juhudi za
kusaidia serikali kwa njia ya utafiti ambapo majibu yanatumiwa
kutengeneza sera au majibu ya changamoto mbalimbali. Mkutano huo
ulifungwa na Waziri Mkuu mstaafu, Mh. Dkt. Salim Ahmed Salim.
Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe Dkt. Philip Mpango akisoma hotuba kwa
niaba ya Makamu wa Rais Mh. Samia Suluhu Hassan (hayupo pichani) wakati
akifungua mkutano wa 6 wa mwaka wa ESRF unaozungumzia biashara na
uwekezaji kati ya Tanzania na China uliofanyika jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Tafiti za Kiuchumi na Kijamii (ESRF),
Dk. Tausi Kida akitoa neno la ukaribisho kwa washiriki wa mkutano wa 6
wa mwaka wa ESRF unaozungumzia biashara na uwekezaji kati ya Tanzania na
China uliofanyika jijini Dar es Salaam.
Mwenyekiti wa bodi ya ESRF, Philemon Luhanjo akizungumza machache kabla
ya kumkaribisha mgeni rasmi kufungua mkutano wa 6 wa mwaka wa ESRF
unaozungumzia biashara na uwekezaji kati ya Tanzania na China
uliofanyika jijini Dar es Salaam.
Mwakilishi wa Ubalozi wa China nchini Tanzania anayeshughulikia wa
Masuala ya Uchumi na Biashara, Lin Zhiyong akizungumza kwa niaba ya
balozi wa China wakati wa ufunguzi wa mkutano wa 6 wa mwaka wa ESRF
unaozungumzia biashara na uwekezaji kati ya Tanzania na China
uliofanyika jijini Dar es Salaam.
Katibu Mkuu Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Profesa Adolf
Mkenda akiwasilisha mada inayohusu namna watanzania wanavyoweza
kunufaika na fursa za kibiashara na uwekezaji China wakati wa mkutano wa
6 wa mwaka wa ESRF unaozungumzia biashara na uwekezaji kati ya Tanzania
na China uliofanyika jijini Dar es Salaam.
Pichani juu na chini ni sehemu ya washiriki kutoka China na Tanzania
waliohudhuria mkutano wa 6 wa mwaka wa ESRF unaozungumzia biashara na
uwekezaji kati ya Tanzania na China uliofanyika jijini Dar es Salaam. Mwenyekiti
ya Taasisi ya Utafiti wa Maendeleo China (CIDRN), Prof. Dr. Li Xiaoyun
akitoa neno la ukaribisho kwa washiriki wa mkutano wa 6 wa mwaka wa ESRF
unaozungumzia biashara na uwekezaji kati ya Tanzania na China
uliofanyika jijini Dar es Salaam.
Balozi wa Tanzania nchini China, Mh. Mbelwa Kairuki akizungumzia namna
ambavyo watanzania wanaweza wakafaidika na fursa za biashara na
uwekezaji nchini China wakati wa mkutano wa 6 wa mwaka wa ESRF
unaozungumzia biashara na uwekezaji kati ya Tanzania na China
uliofanyika jijini Dar es Salaam.
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Anthony Mtaka akiwasilisha mada inayohusu
mahusiano ya kibiashara ya uwekezaji kati ya Tanzania na China kwa
mtazamo wa Serikali za Mitaa wakati wa mkutano wa 6 wa mwaka wa ESRF
unaozungumzia biashara na uwekezaji kati ya Tanzania na China
uliofanyika jijini Dar es Salaam.
Kutoka kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Utafiti wa Uchumi
na Jamii (ESRF), Dk. Tausi Kida, Balozi wa Tanzania nchini China, Mh.
Mbelwa Kairuki, Waziri Mkuu mstaafu, Dkt. Salim Ahmed Salim, Mwenyekiti
wa bodi ya ESRF, Philemon Luhanjo, Mwenyekiti na Afisa Mtendaji Mkuu wa
Kampuni za Infotech Investment, Ali Mfuruki wakifuatilia mada mbalimbali
zilizokuwa zikiwasilisha wakati wa mkutano wa 6 wa mwaka wa ESRF
unaozungumzia biashara na uwekezaji kati ya Tanzania na China
uliofanyika jijini Dar es Salaam. Mkutano ukiendelea.
Balozi wa Tanzania nchini China, Mh. Mbelwa Kairuki pamoja na Waziri
Mkuu mstaafu, Dkt. Salim Ahmed Salim wakifuatilia mada mbalimbali
zilizokua zikiwasilishwa katika mkutano wa 6 wa mwaka wa ESRF
unaozungumzia biashara na uwekezaji kati ya Tanzania na China
uliofanyika jijini Dar es Salaam.
Profesa Humphrey Moshi kutoka idara ya Uchumi katika Chuo Kikuu cha Dar
es Salaam akiwasilisha mada inayohusu uhusiano wa China na Tanzania
katika masuala ya uwekezaji na biashara wakati wa mkutano wa 6 wa mwaka
wa ESRF unaozungumzia biashara na uwekezaji kati ya Tanzania na China
uliofanyika jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka Maalum ya Uwekezaji (EPZA), Kanali Mstaafu
Joseph Simbakalia akichangia maoni wakati wa mkutano wa 6 wa mwaka wa
ESRF unaozungumzia biashara na uwekezaji kati ya Tanzania na China
uliofanyika jijini Dar es Salaam.
Mwanachama wa Chama cha Wanafunzi walisomea China (CAAT), Linas Kahisha
akielezea uzoefu wake katika fursa za kibiashara nchini humo katika
mkutano wa 6 wa mwaka wa ESRF unaozungumzia biashara na uwekezaji kati
ya Tanzania na China uliofanyika jijini Dar es Salaam.
Pichani juu na chini ni washiriki kutoka Tanzania na Chini
waliohudhuria mkutano wa 6 wa mwaka wa ESRF unaozungumzia biashara na
uwekezaji kati ya Tanzania na China uliofanyika jijini Dar es
Salaam.[/caption]
Mgeni rasmi Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe Dkt. Philip Mpango,
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Utafiti wa Uchumi na Jamii (ESRF), Dk.
Tausi Kida na Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Anthony Mtaka wakiwa katika picha
ya pamoja na wanafunzi watafiiti kutoka nchini China.
Mkuu wa Idara ya Utafiti na Machapisho wa ESRF, Prof. Fortunata Makene
(kushoto) katika picha ya kumbukumbu na Mkuu wa Idara ya Maarifa na
Ubunifu wa ESRF, Bi. Margareth Nzuki (kulia) mara baada ya ufunguzi
rasmi wa mkutano wa 6 wa mwaka wa ESRF unaozungumzia biashara na
uwekezaji kati ya Tanzania na China
Mkurugenzi
Mtendaji wa Taasisi ya Utafiti wa Uchumi na Jamii (ESRF), Dk. Tausi
Kida (katikati), Mkuu wa Idara ya Maarifa na Ubunifu wa ESRF, Bi.
Margareth Nzuki na Mwenyekiti ya Taasisi ya Utafiti wa Maendeleo China
(CIDRN), Prof. Dr. Li Xiaoyun katika picha ya kumbukumbu.
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Anthony Mtaka (katikati) katika picha ya pamoja
na washiriki kutoka TPSF na ESRF na Mshereshaji wa mkutano huo Eng.
George Mulamula (kushoto).
Baadhi ya washiriki kutoka China wakichukua baadhi ya makabrasha yenye
taarifa mbalimbali zilizoandaliwa na ESRF wakati wa mkutano wa 6 wa
mwaka wa ESRF unaozungumzia biashara na uwekezaji kati ya Tanzania na
China uliofanyika jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe Dkt. Philip Mpango akisalimiana na
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Utafiti wa Uchumi na Jamii (ESRF), Dk.
Tausi Kida alipowasili katika ufunguzi wa mkutano wa 6 wa mwaka wa ESRF
unaozungumzia biashara na uwekezaji kati ya Tanzania na China
uliofanyika jijini Dar es Salaam.
Mgeni rasmi Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe Dkt. Philip Mpango
(katikati) akiongozana na Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Utafiti wa
Uchumi na Jamii (ESRF), Dk. Tausi Kida (kushoto) na Mwenyekiti wa bodi
ya ESRF, Philemon Luhanjo baada ya kuwasili katika mkutano wa 6 wa mwaka
wa ESRF unaozungumzia biashara na uwekezaji kati ya Tanzania na China
uliofanyika jijini Dar es Salaam.
Mgeni
rasmi Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe Dkt. Philip Mpango katika picha
ya kumbukumbu na Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Utafiti wa Uchumi na
Jamii (ESRF), Dk. Tausi Kida mara baada ya kufungua mkutano wa 6 wa
mwaka wa ESRF unaozungumzia biashara na uwekezaji kati ya Tanzania na
China uliofanyika jijini Dar es Salaam.
No comments:
Post a Comment