Mamlaka
ya Chakula na Dawa Tanzania (TFDA) imetoa mafunzo kwa wasindikaji
wadogo wa vyakula 1287 tangu mwaka 2013 ili waweze kusindika vyaklula
vyenye ubora kwa mujibu wa sheria na kanuni za uzalishaji na kuhimili
ushindani wa soko.
Akifungua
mafunzo ya wasindikaji wadogo wapatao 60 wa vyakula yaliyoratibiwa na
Mamlaka hiyo leo jijini Dar es Salaam kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu wa
Mamlaka hiyo Bw. Hiiti Sillo, Mkurugenzi wa Usalama wa Chakula Bw.
Raymond Wigenge, amesema dhamira ya Serikali ni kuwawezesha
wajasiriamali wadogo hapa nchini.
“Kukua
kwa viwanda hivi kutakuwa na mchango mkubwa katika kuongeza ajira na
kipato katika ngazi ya kaya, kukuza kilimo cha mazao ya chakula kutokana
na kuwepo kwa soko la mazao ya vyakula”. Alisisitiza Wigenge.
Akifafanua
Wigenge amesema Serikali inatambua kuwa viwanda vidogo vina nafasi
kubwa ya kuchangia pato la Taifa hasa katika kipindi hiki ambacho
Serikali inasisitiza ujenzi wa uchumi wa Viwanda.
Alieleza
kuwa Mamlaka hiyo imeingia mkataba wa maridhiano (MOU) na Shirika la
Viwango Tanzania (TBS) ambapo mchango wa taasisi hizo mbili utatambuliwa
katika tasnia ya ujasiriamali wa bidhaa zinazodhibitiwa na Mamlaka.
“Katika
makubaliano tuliyofikia kati ya TFDA na TBS ambapo kuanzia sasa mamlaka
yetu itatumia matokeo ya vipimo vya maabara za TBS kusajili bidhaa
husika na TBS itazingatia usajili wa TFDA wa jengo la bidhaa wakati wa
kutoa alama ya ubora”. Alisisitiza Wigenge.
Akizungumzia
umuhimu wa mafunzo hayo, Mwenyekiti wa Chama Kuweka na Kukopa cha
Wajasiliamali Wadogo Wanawake Tanzania (TASWE) na mwakilishi wa wanawake
wajasiriamali Bi. Anna Matinde amesema kuwa mafunzo kwa wajasiriamali
wadogo yana umuhimu katika kuchochea maendeleo ya Viwanda hapa nchini.
“Sasa
tumeona juhudi za Serikali katika kuwawezesha wajasiriamali wadogo hapa
nchini na tunapongeza hatua hizi ikiwemo kuandaa mafunzo haya na tumeona
kweli kuna mabadiliko makubwa katika kuwawezesha wajasiriamali”.
Alisisitiza Matinde.
Alieleza
kuwa kwa ni vyema wajasiriamali wakaunga mkono juhudi hizo ili waweze
kunufaika na uwezeshwaji unaofanywa na Serikali kwa wajasiriamali wote
bila kujali ni wadogo au wa kati na hata wakubwa.Mada zilizowasilishwa
katika mafunzo hayo ya siku moja ni pamoja na taratibu za usajili wa
majengo ya vyakula, usajili wa vyakula, utaratibu wa utoaji wa alama ya
ubora na teknolojia ya usindikaji wa vyakula.
Mafunzo
hayo yamefanyika katika mikoa ya Dar es Salaam, Pwani, Mwanza, Arusha,
Mbeya, Dodoma, Rukwa, Manyara, Lindi,Mtwara,Tanga, Singida, Iringa,
Kigoma, Kilimanjaro, na Morogoro.
Mkurugenzi
wa Usalama wa Chakula wa Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA) Bw. Raymond
Wigenge akifungua mafunzo ya wasindikaji wadogo wa vyakula (hawapo
pichani) ambayo yaliatibiwa na Mamlaka hiyo leo Jijini Dar es Salaam.
Meneja
wa Ukaguzi na Ufuatiliaji wa Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA) Bw.
Justin Makisi akitoa ufafanuzi kuhusu umuhimu wa mafunzo kwa wasindikaji
wadogo wa vyakula.
Mwenyekiti
wa Chama cha Kuweka na Kukopa Wajasiriamali Wadogo Tanzania (TASWE) na
muwakilishi wa wanawake wajasiriamali Bi. Anna Matinde akipongeza juhudi
za Serikali katika kuwawezesha wajasiriamali wadogo hapa nchini. Kulia
ni Mkurugenzi wa Usalama wa Chakula wa Mamlaka hiyo Bw. Raymond Wigenge
na kushoto ni Afisa Udhibiti Ubora Bi. Prisca Kuela
Baadhi
ya wajasiriamali wakifuatilia mafunzo yaliyoratibiwa na Mamlaka ya
Chakula na Dawa Nchini (TFDA) kwa wasindikaji wadogo wa vyakula.
Mkurugenzi
wa Usalama wa Chakula wa Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA) Bw. Raymond
Wigenge akizungumza kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka hiyo Bw.
Hiiti Sillo wakati wa mafunzo ya wasindikaji wadogo wa vyakula.
No comments:
Post a Comment