Mstahiki
Meya wa Manispaa ya Kinondoni ,Benjamini Sitta akizungumza wakatiwa
kikao cha baraza la Madiwani katika ukumbi wa Manispa ahiyo Magomeni
jijini Dar es Salaam, jana juni 15, 2017.
Mkurugenzi wa Manispaa ya Kinondoni ,Aron Kangurumjuli aakizungumza wakati wa kikao cha Baraza la Madiwani.
Diwani wa Kata ya Magomeni, Julian Bujugo akichangaia katika Mkutano wa Baraza la Madiwani Kinondoni.
Afisa
Utumishi wa Manispaa ya Kinondoni, Anna Mwakasyesye akijibu hoja za
Madiwani wa Manispaa ya Kinondoni katika kikao cha baraza.
Sehemu ya Madiwani walioshiriki katika kikao cha Baraza la Madiwani la Manispaa ya KINONDONI.
Diwani
wa Kata ya Kunduchi kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi, Michael Urio
akichangia hoja katika kikao cha Baraza la Madiwani kilichofanyika
katika ukumbi wa Manispaa hiyo Magomeni jijini Dar es Salaam.
Diwani
wa kata ya Mwananyamala, Songoro Mnyonge akichangia mada katika kikao
cha Baraza la Madiwani kilichofanyika katika ukumbi wa Manispaa hiyo
Magomeni jijini Dar es Salaam
Mchumi
wa Manispaa ya Kinondoni, Eugene Haruna akijibu hoja za madiwani katika
kikao cha baraza la Madiwani wa Manispaa ya KINONDONI
Mkuu wa kitengo cha Usimamizi wa Manunuzi (PMU) manispaa ya Kinondoni akijibu hoja za Madiwani wa Manispaa hiyo
Diwani
wa kata ya Ndugumbi Manispaa ya Kinondoni ,Thadey Massawe akichangia
hoja katika kikao cha Baraza la Madiwani wa Manispaa ya Kinondoni.
Mstahiki
Meya wa Manispaa ya Kinondoni ,Benjamini Sitta akijadili jambo na
Mkurugenzi wa Manispaa ya Kinondoni ,Aron Kangurumjuli katika kikao cha
Baraza la Madiwani.
Diwani wa Viti Maalum CHADEMA, Caroline Kazinza akichangia hoja katika kikao cha Baraza la Madiwani wa Manispaa ya Kinondoni.
Na Yusuph Mlandula
Baraza
la Madiwani la Manispaa ya Kinondoni limeagiza kuhakikisha fedha zote
zilizopo katika akaunti za kata zaidi ya Bilioni 4.9 zifanyiwe utaratibu
wa manunuzi ili ziweze kutekeleza miradi iliyokusudiwa katika kata
hizo.
Maazimio
hayo yamefikiwa katika baraza la Madiwani wa Manispaa hiyo lililongozwa
na Mstahiki Meya wa Manispaa hiyo, Benjamini Sitta .
Aidha
baraza hilo pia limeridhia maombi ya kamati ya Fedha kwa kutaka kubuni
vyanzo vipya vya fedha vitakavyosaidia Halmashauri hiyo kupata fedha
zaidi licha ya baadhi ya vyanzo kuhamia serikali kuu.
pia
kikao hicho kilipitisha azimio la kumpongeza Rais John Pombe Magufuli
kwa kitendo chake cha kizalendo cha kuhakikisha kuwa fedha za watanzania
zilikuwa zinapotea kutokana na mchanga wa Madini uliokuwa ukisafirishwa
nje kiholela unapangiwa utaratibu wa kunufaisha Serikali.
No comments:
Post a Comment