SERIKALI
ya mkoa wa Tabora imesema haitasita kuchukua hatua za kisheria kwa mtu
yoyote atakayebainika kuendesha vitendo vya uharibifu wa ardhioevu kwa
kuendesha shughuli za kibinadamu kama kilimo, ufugaji mifugo, uchomaji
mkaa na uchomaji moto hovyo kwenye vyanzo vya maji na hifadhi za misitu.
Kauli
hiyo imetolewa na Mkuu wa mkoa wa Tabora Aggrey Mwanri mara baada ya
kushiriki kampeni ya upandaji na umwagiliaji wa miti ambalo ziliendeshwa
na vijana 600 wa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) Msange ambao wametekeleza
agizo la Makamu wa Rais kwa vitendo .
Alisema
kuwa viongozi wote wanatakiwa kushirikiana na wananchi katika kuwabaini
wote wanaoendesha shughuli hizo ovu katika mistu mkoani hapo kwa kuwa
wanahatarisha wakazi wa Tabora na mikoa jirani.
Mkuu
huyo wa Mkoa aliwashukuru vijana hao wa JKT waliomba kushiriki katika
zoezi la kupanda miti kabla ya kumaliza mafunzo yao Jumamosi ili iwe
alama ya uwepo wao katika eneo hilo.
Alisema
kuwa kitendo walichoufanyia vijana hao kimeonyesha jinsi walifundishwa
vizuri juu ya kuwa wazalendo kwa Taifa lao na kitabaki katika kumbukumbu
za Mkoa huo na majina yao yataandikwa.
Akizungumza
wakati wa zoezi hilo Mmoja Mdau wa Mazingira na Mkurugenzi Mtendaji wa
Kuja na Kushoka Bw. Leonard Kushoka alisema kuwa chanjo kikubwa cha
uharibifu wa mazingira ni ukaushaji wa tumbaku kwa kutumia Mabani ya
kizamani na matumizi ya mkaa wa miti kama nishati ya kupikia.
Alisema
kuwa ili tumbaku iweze kukauka katika heka moja unahitaji kilo 10,000
za kuni kwa msimu mmoja kwa mabani ya kizamani wakati ya kisasa mkulima
anahitaji kilo 5,0000
Bw.
Kushoka alisema kuwa hali hiyo inasababisha miti mingi kukatwa kila
mwaka na kuongeza iwapo mistu ya Tabora kwingineko iweze kunusurika
inabidi wakulima waanze kutumia mashine maalum ambayo inatumia mkaa
uliozalishwa na taka katika kuendesha zoezi la kukaushia tumbaku.
Mkuu
wa Mkoa wa Tabora Bw. Aggrey Mwanri akizungumza na waandishi wa habari
jana kabla ya kuanza zoezi la kuondoa magugu katika miti iliyopandwa
katika Manispaa ya Tabora juzi.
Mkuu
wa Mkoa wa Tabora Bw. Aggrey Mwanri akishirikiana na askari wa Kujenga
Taifa(JKT) Msange wanaohitimu mafunzo yao Jumamosi wakati wa zoezi la
kuondoa magugu katika miti iliyopandwa katika Manispaa ya Tabora juzi.
No comments:
Post a Comment