Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais,
Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OR – TAMISEMI), George Simbachaweni
akizungumza na menejimenti za Shirika la Masoko Kariakoo na Shirika la
Maendeleo la Jiji la Dar es Salaam (DDC) wakati wa ziara yake katika ofisi za
mashirika hayo leo jijini Dar es Salaam.Kutoka kushoto ni Mwenyekiti wa Bodi ya
Shirika la Masoko Kariakoo Dkt. Hoseana Bohela Lunogelo.
Mkurugenzi wa Jiji la Dar es
Salaam Bi. Sipora Liana akifafanua jambo wa mbele ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya
Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OR – TAMISEMI) George Simbachawene
(mbele) alipokuwa katika ziara ya kikazi kutembelea Shirika la Masoko Kariakoo
na Shirika la Maendeleo la Jiji la Dar es Salaam (DDC) leo.
Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika la
Masoko Kariakoo Dkt. Hoseana Bohela Lunogelo akielezea jambo mbele ya Waziri wa
Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OR – TAMISEMI)
George Simbachawene (kulia) wakati wa ziara ya kikazi ya Waziri huyo katika
Shirika la Masoko Kariakoo na Shirika la Maendeleo la Jiji la Dar es Salaam
(DDC) leo. Katikati ni Mstahiki Meya wa Jiji la Dar es Salaam, Isaya Mwita.
Baadhi ya wajumbe wa Bodi ya
Shirika la Maendeleo la Jiji la Dar es Salaam(DDC) wakifuatilia maelekezo ya
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OR –
TAMISEMI), George Simbachaweni(hayupo pichani) wakati wa ziara ya kikazi katika
Mashirika ya Masoko Kariakoo na Shirika la Maenedeleo la Jiji la Dar es Salaam
(DDC).
Mstahiki Meya wa Jiji la Dar es
Salaam Isaya Mwita (kushoto) akimuongoza Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Tawala
za Mikoa na Serikali za Mitaa (OR – TAMISEMI), George Simbachaweni(mwenye suti
nyeusi) kuelekea katika Ofisi za Shirika la Maendeleo la Jiji la Dar es Salaam
(DDC) wakati wa ziara ya kikazi kutembelea Shirika hilo pamoja na Shirika la
Masoko Kariakoo leo Jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OR – TAMISEMI), George Simbachaweni akizungumza na wafanyabiashara wadogowadogo maarufu kama Machinga wanaopanga bidhaa zao mbele ya Ofisi za Shirika la Maendeleo la Jiji la Dar es Salaam wakati wa ziara ya kikazi kutembelea Shirika hilo pamoja na Shirika la Masoko Kariakoo leo Jijini Dar es Salaam.
Serikali imeipongeza Bodi
na Menejimenti nzima ya Shirika la Maendeleo la Jiji la Dar es Salaam (DDC) kwa
juhudi zao zakurejesha uhai wa Shirika hilo richa ya changamoto wanazo kumbana
nazo.
Pongezi hizo zimetolewa na
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OR
–TAMISEMI), George Simbachawene wakati akipokea taarifa fupi ya Shirika la
Maendeleo la Jiji la Dar es Salaam (DDC) na Shirika la Masoko Kariakoo
alipokutana na menejinti ya mashirika hayo leo.
Waziri Simbachawene alisema
kuwa amepitia taarifa ya Shirika hilo na kuridhika nayo hivyo hana budi
kuipongeza timu nzima ya uongozi kwani kwa muda mfupi imeweza kufanya
mabadiliko na kuweza kuliinua tena Shirika hilo.
“Pamoja na kuipongeza bodi
hii lakini napenda kuwashauri kuangalia maeneo mengine ya kuwekeza kama
kufungua maeneo mengi zaidi ya burudani kwani hilo ndilo lilikuwa lengo la
kuanzishwa kwa DDC,ikiwa ni pamoja na kuweka mahali ambapo watoto wataweza
kucheza ili kuhakikisha shirika linajiongezea kipato na kuiongezea Serikali
kipato pia,” alisema Waziri Simbachawene.
Simbachawene alitumia
nafasi hiyo kuwaagiza Wakuu wa Mashirika ya Masoko Kariakoo na Shirika la
Maendeleo la Jiji la Dar es Salaam kuhakikisha wanaandaa taarifa nyingine
itakayohusisha mali zote za mashirika hayo.
Aidha ameutaka uongozi wa
Shirika la Masoko Kariakoo kuwa wabunifu kwa kuanzisha masoko sehemu mbalimbali
za Jiji la Dar es Salaam ikiwa ni mkakati wa kusogeza huduma kwa wananchi na
njia ya kuongeza ajira kwa vijana.
Alilitaka Shirika hilo
kuachana na mawazo ya kizamani na badala yake wajipange kimkakati ili kuendana
na wakati ikiwemo kufikiria namna ya kuwaza kushusha mizigo katika soko hilo
kwani serikali haitaweza kuruhusu maroli ya mizigo kufika katika soko hilo ili
kupunguza ya kuepuka msongamano katikati ya jiji.
Aliushauri uongozi huo
uandae mikakati ya kuwezesha soko hilo kuwa la kiwango cha juu (Super Market)
na kuwalipisha wafanyabiashara kiwango kinachoendana na bei halisi ya soko kama
ambavyo wapangishaji wengine wamekuwa wakitoza ili kukuza kipato kwa Taifa.
Waziri Simbachawene
ameahidi kushirikiana na mashirika hayo katika kutatua changamoto ambazo
zinahitaji msaada wa uongozi na kuwataka wafanye kazi kwa bidii kwani Serikali
ya Awamu ya Tano inahitaji watu wanaojituma na kuchapa kazi.
Awali akiwasilisha taarifa
fupi ya Shirika la Maendeleo la Jiji la Dar es Salaam Meneja Mkuu wa Shirika
hilo Rwandiko Manumbu alisema kuwa pamoja na changamoto wanazokumbana nazo
Shirika limefanikiwa kutoa shilingi milioni 140/- kama gawio kwa mwanahisa wake
ambaye ni Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam.
“Mhe. Waziri, kwa mara ya
kwanza tangu kuanzishwa kwa Shirika hili tumeweza kutoa gawio la kiasi cha
shilingi milioni 140/- kwa Halmashauri ya Jiji na haya ni mafanikio makubwa
kwetu,” alisema Manumbu.
Kwa upande wake Mstahiki
Meya wa Jiji la Dar es Salaam, Isaya Mwita amempongeza Waziri Simbachawene kwa
utayari wake wa kushughulikia changamoto zinazo yakabli mashirika hayo ikiwa ni
pamoja na kutenga muda wake kuja kusikiliza matatizo yao.
Pamoja na pongezi hizo
Mwita alishauri Shirika la Maendeleo la Dar es Salaam (DDC) kuangalia uwezekano
wa kurejesha bendi za muziki kama ambavyo Hayati Baba wa Taifa, Mwalimu Julius
Nyerere alivyokuwa amedhamiria wakati wa uanzishwaji wa Shirika hili.
Shirika la Maendeleo la
Jiji la Dar es Salaam (DDC) na Shirika la Masoko Kariakoo ni mashirika ya Umma
yanayoongozwa na Serikali kupitia Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam chini ya
Sheria za Makampuni namba 2012 ya mwaka 1971 na Sheria ya Bunge namba 36 ya
mwaka 1974, “The Kariakoo Market Corporation Act, 1974
No comments:
Post a Comment