Watoto watatu wa shule ya msingi ya Lucky Vicent
walionusurika katika ajali ya basi, wamefanyiwa upasuaji na sasa wapo wodini
wakiendelea na mazoeazi, ila Doreen, jana alipewa MAPUMZIKO maalumu akiwa
anaandaliwa tayari kwa UPASUAJI wa uti wa mgongo 'spine' unaofanyika leo.
Mbunge wa Singida
Kaskazini, Lazaro Nyalandu aliyeshiriki katika kuwasafirisha watoto hao,
ameandika katika ukurasa wake wa facebook akisema watoto hao kwa sasa wamewekwa
kwenye vyumba vya peke yao.
Upasuaji huo umefanyika
katika Hospitali ya Mercy, Sioux City, Marekani.
Amefafanua upasuaji
waliofanyiwa na kusema mtoto Saidia alifanyiwa upasuaji wa mfupa wa kulia wa
nyonga, mkono wa kulia na kuwekewa ngao kwenye shingo atakayotakiwa kukaa nayo
kwa wiki sita.
“Kwa upande wa mtoto
Wilson, yeye amefanyiwa upasuaji wa nyonga ya kulia, kiwiko cha kulia kilichokuwa
kimevunjika mara tatu na kiwiko cha kushoto,” amesema
Amesema Doreen yeye
amefanyiwa upasuaji wa nyonga, taya katika upasuaji uliochukua saa nne.
Leo Doreen atafanyiwa
upasuaji wa uti wa mgongo.




No comments:
Post a Comment