A great place to access the latest news and information.

Breaking

Post Top Ad

Your Ad Spot

Monday, May 29, 2017

Everton kukipiga Uwanja wa Taifa!

Klabu ya nchini Uingereza ya Everton inatarajia kutembelea Tanzania na kucheza mechi za kujiandaa na msimu mpya wa 2017/18.

Taarifa iliyoripotiwa na tovuti ya klabu hiyo imesema Everton watatembelea Tanzania na itakuwa timu ya kwanza ya Ligi Kuu ya England kucheza mechi katika nchi za Afrika Mashariki.

Ziara hiyo ambayo itakuwa sehemu ya sherehe zao za udhamini mpya wa Kampuni ya SportPesa, itaifikisha Everton kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam wenye uwezo wa kubeba mashabiki 60,000 kucheza mechi Alhamisi ya Julai 13.

Everton imemaliza ya saba katika msimamo wa Ligi Kuu ya England ikijikusanyia jumla ya pointi 61 huku Chelsea ikimaliza ya kwanza kwa kuwa na pointi 93 katika ligi hiyo inayoshirikisha timu 20.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages