Daktari
bingwa wa pua na masikio kutoka China Dk. Fei Jie, akimfanyia uchunguzi wa pua
Bi. Amina Himid katika siku ya Afya
ya kijiji iliyofanyika Shule ya Kwamtipura
Daktari bingwa kutoka Jamhuri ya Watu wa China Dk. Gao, akimpima kifua mtoto Salma Mohammed mkazi wa Kilmahewa, katika siku ya Afya ya Kijiji iliyofanyika Shule ya Kwamtipura Wilaya ya Mjini Unguja.
Afisa Afya akimpatia dawa mmoja wa wagojwa waliofika kupata huduma katika siku ya afya ya kijiji huko Skuli ya Kwamtipura Wilaya ya Mjini.
Vijana
wakiwa kwenye foleni wakisubiri kuonana na daktari kwa ajili ya uchunguzi.
Wananchi waliojitikeza kupatiwa huduma katika siku ya Afya ya Kijiji huko Shule ya Kwamtipura.
Watoto
wakinywa Uji mara baada ya kupatiwa huduma za afya.
Mkurugenzi wa Kinga na elimu ya afya Dk. Fadhil
Mohammed Abdalla, amewataka wananchi wajitokeze kwa wingi kupima afya zao.
Amesema hatua hiyo ni muhimu kwani humuwezesha mtu
kubaini mapema iwapo amepata maradhi na hivyo kutibiwa kabla athari haijwa
kubwa.
Akizungumza na waandishi wa habari leo wakati wa
kutolewa huduma za afya katika shehia ya Kilimahewa Bondeni kutoka kwa
madaktari bingwa wa China, amesema kuwa ni vyema kunapotokea fursa ya huduma
bila malipo, wananchi wazichangamkie ipasavyo.
Dk. Fadhil alisema serikali imekuwa ikichukua
juhudi kubwa kuwafikishia wananchi huduma za afya karibu na maeneo yao
wanakoishi.
“Huduma hii adhimu na ni muhimu kwa kujua afya yako
na baada ya kupata vipimo unapata matibabu na wengine hushauriwa wafike
hospitali ya Mnazi mmoja kwa kupata matibabu zaidi.” Alisema mkurugenzi huyo.
Dk. Fadhil amesema lengo la huduma hizo ni
kuwashajiisha wananchi waweze kuelewa maradhi waliyonayo na kuwezesha kupatiwa
matibabu.
Aidha alieleza kuwa, madaktari hao hutoa elimu ya
afya kuhisiana na maradhi ya kuambukiza hasa katika kipindi hichi cha mvua.
Nae daktari dhamana wa wilaya ya mjini Ramadhani
Mikidadi Suleiman, amesema zoezi la kupima afya ni muhimu na wataalamu wa kutosha
wapo hivyo wananchi wasipuuze kujitokeza.
Katika uchunguzi uliofanya kweny zoezi hilo, Dk.
Mikidadi alisema wananchi wengi wamegundulika na matatizo ya macho, meno, koo,
kisukari na shinikizo la damu na kupatiwa matibabu.
Amewahimiza wananchi kutodharau zoezi hilo
litakalokuwa linafanyika kila baada ya miezi mitatu.
Naye sheha wa shehia ya Kwamtipura Hassan Hashir
Hassan, ameeleza kufurahika kwake kutokana na wananchi wengi kuitikia wito na
kujitokeza katika zoezi hilo lililofanyika bila ya malipo.

No comments:
Post a Comment