A great place to access the latest news and information.

Breaking

Post Top Ad

Your Ad Spot

Thursday, April 20, 2017

WATU 13 WATAKIWA KUFIKA KITUO CHA KATI WAKIWA NA MITAMBO YAO YA KUZALISHA KAZI ZA WASANII

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda amewataja watu 13 wenye mitambo ya kufyatua kazi za wasanii wa nje na ndani ya nchi yetu  wakutane kituo cha polisi cha kati wakiwa na nyaraka halali za kufanyia kazi hiyo.

 Akizungumza na wasanii hao pamoja na wananchi leo katika mkutano wa kupambana na maharamia wa kazi za wasanii,Makonda alisema kuna baadhi ya watu wanafanya kazi za bla bla kwa kuwanyonya wasanii.

Amesema kuanzia leo ni mwisho kwa wale wanaouza nyimbo za wasanii amesema wanaotakiwa kufanya hivyo niwale wenye mikataba halali na wasanii wenye nyimbo husika.

Makonda amesema kuwa kazi zote za wasanii na zinatakiwa ziwe na stika za Mamlaka ya Mapato nchini (TRA) ilinchi iweze kupata mapato na kukuza tasnia ya sanaa nchini.

Amesema kwa wale wanaouza kazi za wasanii mikononi zinatakiwa kuwa na stika za TRA Pamoja na kuwa na kibali maalum kutoka bodi ya filamu

Hata hivyo amesema Makonda kunawatu wanafanya kazi za kuwarubuni wasanii na kufanya maisha yao yawe duni katika hiyo wakati Nigeria inaongoza kwa kupata pesa nyingi kupitia filamu


Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda akizungumza na wasanii katika mtaa wa Mafya mara baada ya kumaliza maandamano ya wasanii kupinga uuzwaji wa filamu za nje ambazo zinachangia kushuka kwa thamani ya filamu za ndani kutokana na bidhaa hizo kutolipiwa kodi.

Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Sophia Mjema akizungumza na Wasanii waliofika Kariakoo mara baada ya maandamano ya kupinga Biashara ya uuzaji filamu za nje.
Katibu Mtendaji wa Baraza la Sanaa nchini (BASATA), Godfrey Mwingereza akizungumza na wasanii wa filamu waliofika katika maandamano hayo yaliyoitimishwa katika mtaa wa Mafia Kariakoo.

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda akiwa katika maandamano na wasanii wa filamu hapa nchini kupinga uuzwaji wa filamu za nje nchini ambazo hazilipiwi ushuru
Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Simon Sirro akizungumza na Wasanii hao.
Makamu Mwenyekiti wa Shirikisho la Filamu nchini, Jimy Mafufu akizungumza kwa niaba ya wasanii katika mkutano huo.
 Baadhi ya wasanii walishiriki Maandamano hayo
Kundi la Wasanii wakishangilia jambo kutoka kwa mkuu wa Dar es Salaam Paul Makonda

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages