Meneja
Masoko wa kampuni ya Sun King nchini Tanzania, Albert Msengezi, akizungumza na
wanahabari kwenye uzinduzi rasmi wa ofisi na bidhaa za Sun King nchini,
uliofanyika hii leo Buzuruga Plaza Jijini Mwanz
Mkuu wa Masoko wa
kampuni ya Sun King Tanzania, Judie Wu, akizungumza kwenye uzinduzi rasmi
wa ofisi na bidhaa za Sun King nchini Tanzania, uliofanyika Buzuruga Plaza
Jijini Mwanza hii leo.
Mgeni Rasmi, Afisa Tawala wilaya ya Nyamagana mkoani
Mwanza, Zubeda Kimaro, akizungumza kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, John
Mongella, kwenye uzinduzi rasmi wa ofisi na bidhaa za Sun King nchini Tanzania,
uliofanyika Buzuruga Plaza Jijini Mwanza hii leo.
Afisa Tawala wilayani Nyamagana, Zubeda Kimaro
(mwenye kofia), akizindua ofisi ya Sun King Jijini Mwanza ikiwa ni uzinduzi
rasmi wa kampuni hiyo kimataifa hii leo. Kulia ni Mkuu wa Masoko wa
kampuni ya Sun King Tanzania, Judie Wu.
Wakazi wa
maeneo ambayo bado hayajafikiwa na huduma ya umeme nchini, wanatarajiwa
kunufaika na huduma hiyo kupitia mitambo ya umeme wa jua kwa bei nafuu
inayosambazwa na kampuni ya Sun King.
Meneja Masoko
wa kampuni hiyo nchini, Albert Msengezi, ameyabainisha hayo hii leo Jijini
Mwanza kwenye uzinduzi rasmi kitaifa wa bidhaa za Sun King ambazo ni taa za
sola pamoja na majiko bunifu ya Jikokoa.
“Kila Kijiji
nchini tunakusudia kuwa na mawakala wa kampuni ya Sun King ambao watawafikia
wananchi wote wanaoishi katika maeneo hayo na hadi kufikia mwishoni mwa mwaka
huu tunakusudia kuwa na wanufaika zaidi ya Milioni Moja ambapo tumejikita
kwenye bidhaa bora zisizochafua mazingira ikiwemo taa za sola na majiko
yasiyochafua mazingira”. Amebainisha Msengezi.
Mkuu wa
Masoko wa kampuni ya Sun King, Judie Wu, amesema kampuni hiyo imedhamiria
kuhakikisha kila mmoja Mjini na Vijijini anapata huduma ya umeme pamoja na
kutumia majiko bunifu yasiyo na madhara kiafiya kwa bei nafuu.
Akizungumza kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Mwanza
kwenye uzinduzi huo wa bidhaa za King Sung, Zubeda Kimaro ambaye ni Afisa
Tawala wilayani Nyamagana, amewahimiza wawekezaji kujitokeza kwa wingi kuwekeza
mkoani Mwanza kwani kuna fursa nyingi za kiuwekezaji hatua ambayo pia
itazalisha ajira zaidi kwa vijana wetu
No comments:
Post a Comment