Meneja wa Benki ya NMB Kanda ya
Dar es salaam na Pwani, Vick Bishubo (kulia) akizungumza kwenye mkutano wa
wafanyabiashara wa Dar es Salaam "NMB Business Club' waliokutanishwa na
benki hiyo jana jijini Dar es Salaam kwa lengo la kutoa mafunzo ya biashara
pamoja na kodi ili kukuza biashara zao.
Afisa Mkuu wa NMB Kitengo cha
Wateja wadogo na wakati, Abdulmajid Nsekela (kulia) akizungumza kwenye mkutano
wa wafanyabiashara wa '"NMB Business Club' waliokutanishwa na NMB jana
jijini Dar es Salaam kwa lengo la kutoa mafunzo ya biashara pamoja na kodi ili
kukuza biashara zao.
Baadhi ya wafanyabiashara
walioshiriki mkutano huo wakizungumza kuelezea mafanikio yao juu ya huduma za
mikopo na ukuaji wa biashara zao.
BENKI ya NMB imekutanisha
wafanyabiashara zaidi ya 500 wa jijini Dar es Salaam waliopo katika jumuia ya
wafanyabiashara wa NMB "NMB Business Club" kwa lengo la kutoa mafunzo
mbalimbali ya biashara pamoja na mafunzo ya kodi ili kukuza biashara zao.
Kundi hilo la NMB Business Club
mkoa wa Dar es Salaam limekutanishwa kwa pamoja ili wafanyabiashara hao waweze
kujuana na kubadilishana uzoefu katika shughuli zao jambo ambalo litachangia
wao kushikamana na kunufaika zaidi na huduma zinazotolewa na benki hiyo.
Akizungumza na wafanyabiashara
katika mkutano huo, Afisa Mkuu wa NMB Kitengo cha Wateja wadogo na wakati,
Abdulmajid Nsekela alisema katika semina hiyo wataalam wa biashara wa Benki ya
NMB watatoa mafunzo mbalimbali ya namna ya kukuza biashara na kuelezea fursa
anuai zilizopo ndani ya benki hiyo ili wateja wao waendelee kunufaika nazo.
Alisema mbali ya kutoa mafunzo ya biashara na kodi wana NMB Business Club
walioshiriki katika mkutano huo watapata fursa ya kutoa mrejesho dhidi ya
huduma wanazopewa ili benki iangalie namna ya kuzishughulikia.
Sehemu ya wafanyabiashara
walioshiriki mkutano huo.
Baadhi ya wafanyabiashara walioshiriki mkutano huo
wakizungumza kuelezea mafanikio yao juu ya huduma za mikopo na ukuaji wa
biashara zao.
Sehemu ya wafanyabiashara
walioshiriki mkutano huo.
Awali mgeni rasmi ambaye ni Mkurugenzi wa Jiji la
Dar es Salaam, Spora Liana akifungua mkutano huo aliwataka wafanyabiashara hao
kutambua kuwa Serikali inawategemea wafanyabiashara katika kukuza jiji kupitia
huduma mbalimbali za kibiashara ambzo wanazitoa kwa jamii.
Alisema Serikali kupitia ofisi yake itaendelea
kujenga mazingira bora ya wafanyabiashara kuendesha biashara zao kwa maendeleo
na kuwaomba walipe kodi kama inavyotakiwa kwenye biashara zao, kwani hii ndio
njia pekee ya kuboresha huduma na maendeleo kwa jamii.
"...Mtambue ya kwamba katika huduma mnazozitoa
kibiashara mbali ya kunufaika nyinyi mnachangia kuleta maendeleo, pia
mnapendezesha jiji letu...inapaswa mtambue ni watu muhimu sana katika kujenga
uchumi," alisema Mkurugenzi huyo wa jiji la Dar es Salaam. Kwa upande wake
Kaimu Mwenyekiti wa NMB Business Club Mkoa wa Dar es Salaam, Ezekiel Gutti
alisema wafanyabiashara walioalikwa katika mkutano huo ni ambao wamekuwa
wakinufaika na huduma mbalimbali za mikopo na ushauri wa kifedha kutoka kwa
benki ya NMB na wanafanya vizuri katika biashara zao na hata marejesho kwa
mikopo mbalimbali wanayoomba benki.
Mkurugenzi
wa Jiji la Dar es Salaam, Spora Liana akizungumza kufungua mkutano wa
wafanyabiashara wa Dar es Salaam "NMB Business Club' waliokutanishwa na
benki hiyo jana jijini Dar es Salaam kwa lengo la kutoa mafunzo ya biashara
pamoja na kodi ili kukuza biashara zao.
Afisa
Mkuu wa NMB Kitengo cha Wateja wadogo na wakati, Abdulmajid Nsekela (kulia)
akizungumza kwenye mkutano wa wafanyabiashara wa '"NMB Business Club'
waliokutanishwa na NMB jana jijini Dar es Salaam kwa lengo la kutoa mafunzo ya
biashara pamoja na kodi ili kukuza biashara zao.
Afisa
Mkuu wa NMB Kitengo cha Wateja wadogo na wakati, Abdulmajid Nsekela akizungumza
na wanahabari (hawapo pichani) kwenye mkutano wa wafanyabiashara wa "NMB
Business Club' waliokutanishwa na NMB jana jijini Dar es Salaam kwa lengo la
kutoa mafunzo ya biashara pamoja na kodi ili kukuza biashara zao. Takribani
wafanyabiashara zaidi ya 500 walishiriki mkutano huo wa mafunzo ya biashara
jijini Dar es Salaam.
Mwenyekiti
wa NMB Business Club Mkoa wa Dar es Salaam, Ezekiel Gutti akizungumza na
wanahabari (hawapo pichani) kwenye mkutano wa wafanyabiashara wa '"NMB
Business Club' waliokutanishwa na NMB jana jijini Dar es Salaam kwa lengo la
kutoa mafunzo ya biashara pamoja na kodi ili kukuza biashara zao. Takribani
wafanyabiashara zaidi ya 500 walishiriki mkutano huo wa mafunzo ya biashara
jijini Dar es Salaam.
Sehemu
ya wafanyabiashara walioshiriki mkutano huo.
No comments:
Post a Comment