A great place to access the latest news and information.

Breaking

Post Top Ad

Sunday, April 30, 2017

Uchaguzi wawakilishi wa Chadema Bunge la Afrika Mashariki (EALA) Kufanyika Mei 10




Bunge limetangaza kuwa, uchaguzi mdogo wa kupata wawakilishi wawili wa nafasi ya ubunge kwa Bunge la Afrika Mashariki (EALA) kutoka Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), sasa utafanyika Mei 10, mwaka huu kwenye ukumbi wa Bunge, mjini Dodoma.

Kwa mujibu wa taarifa ya Katibu wa Bunge ambaye pia ni Msimamizi wa Uchaguzi huo, Dk Thomas Kashilillah, uteuzi wa wagombea utafanyika Mei 3. 

Watakaopigiwa kura na kuchaguliwa katika uchaguzi huo wataungana na wengine saba, sita wakiwa kutoka Chama Cha Mapinduzi (CCM) na mmoja kutoka Chama cha Wananchi (CUF) ambao walishinda katika uchaguzi wa Aprili 4, mwaka huu.

Siku hiyo, Chadema licha ya kuweka wagombea wao Lawrence Masha na Ezekiah Wenje, kura zao hazikutosha hivyo kukosa sifa za kuchaguliwa. 

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Pages