Katibu
Tawala wa Mkoa wa Mbeya Bibi Mariam Mtunguja akiongea wakati wa ufunguzi wa
mkutano kati ya kikosi kazi cha Kitaifa cha kunusuru ikolojia ya mto Ruaha
pamoja na Wananchi wa Kata ya Madibira wilayani Mbarali Mkoani Mbeya.
Sehemu
ya Wananchi waliohudhuria mkutano huo wakifuatilia kwa makini mkutano huo.
Halimashauri ya Wilaya ya
Mbalari imeagizwa kuhakikisha ng’ombe wote wa Wilaya hiyo wanawekewa chapa ili
kurahisisha kuweza kujua ng’ombe wote wa Wilaya hiyo. Pia kila mfugaji awe na
ng’ombe wasiozidi arobaini tu ili kuweza kuzuia uharibifu wa mazingira
uanaosababibshwa na mifugo wengi kupita kiasi. Katika maagizo hayo pia
Halimashauri ya Wilaya ya Mbarali imetakiwa kushirikiana na Wananchi wake
kujenga malambo ya kunyweshea mifugo ili kuepuka uharibifu mkubwa wa mazingira
unaosababishwa na kuingizwa kwa mifugo katika mto Ndembela kwa ajili ya kunywa
maji.
Maagizo hayo yametolewa
na Mwenyekiti wa Kikosi kazi cha Kitaifa cha kunusuru Mto Ruaha ambaye pia ni
Mkurugenzi wa Idara ya Mazingira katika Ofisi ya Makamu wa Rais, Bwana Richard
Muyungi alipokua akiongea na Wananchi wa kata ya Madibira wakati wa mkutano na
Wananchi juu ya kujua na kufahamu changamoto mbalimbali zinazosababaisha
uharibifu wa mazingira katika vyanzo vya maji katika mito inayozunguka Mto wa
Ruaha Mkuu ukiwemo mto Ndembela.
Akiongea katika Mkutano
huo Bwana Muyungi pia ameahaidi kushughulikia Wawekezaji ambao siyo waaminifu
wanaotumia maji bila kibali cha Serikali au wale ambao wanazidisha kiwango cha
uchukuaji maji tofauti na kile kilichoanishwa katika kibali. Alisema kuwa Ofisi
ya Makamu wa Rais inaratibu na kuhakikisha rasilimali zote zilizopo Nchini
zinatumika kwa usahihi.
Akijibu hoja hizo Mhe.
Diwani wa Kata ya Madibira kwa niaba ya Mkurugenzi aliahidi Halimashauri hiyo
kuyafanyia kazi mambo yote waliyoagizwa kuyafanya. Aliongeza kuwa atasimamia
yote na pia atashirikiana na Wananchi wa Madibira kuhakikisha maagizo yote yanapatiwa
ufumbuzi.
Baada ya Mkutano huo pia
Wajumbe wa Kikosi kazi hiko walipata fursa ya kutembelea shamba la mpunga la
chama cha Wanaushirika Madibira (MAMCOS) kwenda kujionea shughuli mbalimbali za
utunzaji wa maji kwa ajili ya kilimo zinavyofanyika. Akiongea baada ya
kutembelea shamba hilo la hekta 3000, Katibu Tawala wa Mkoa wa Mbeya Bibi
Mariam Mtunguja aliwapa agizo la kuweka geji itakayodhibiti kiasi cha maji
yanayotoka shambani baada ya matumizi ya umwagiliaji kufanyika.
Pia wametakiwa
kutengeneza miundo mbinu shambani ili kuwezesha barabara ya shambani hapo
kupitika kwa urahisi na maji kutomwagika hovyo. Pia kusafisha shamba lao mara
moja kuondoa nyasi na magugu yalioota kwenye mifereji ya kupitishia maji
shambani hapo.
Kikosi hiko cha Kitaifa
cha kunusuru ikolojia ya Mto Ruaha Mkuu kiliundwa na Makamu wa Rais wa Tanzania
kikijumuisha Wajumbe kutoka Idara na Taasisi mbalimbali za Serikali. Kikosi
kazi hiko kimegawanyika katika makundi matatu Iringa, Mbeya na Njombe.


No comments:
Post a Comment