A great place to access the latest news and information.

Breaking

Post Top Ad

Your Ad Spot

Wednesday, April 19, 2017

GWIJI LA UIGIZAJI FILAMU MAREKANI AFARIKI




Mwigizaji Clifton James, aliyeigiza kama Liwali JW Pepper kwenye filamu mbili za James Bond, amefariki dunia akiwa na miaka 96.

Alifariki karibu na mji wake aliokulia wa Gladstone, Oregon, siku ya Jumamosi kutokana na matatizo ya ugonjwa wa kisukari.

James alizaliwa mwaka1920 akiwa ni mtoto wa kwanza Bi Grace na Bw Harry James na kufariki tarehe 16 April 2017.


James alifahamika sana kutokana na uigizaji wake pamoja na Sir Roger Moore katika filamu za Bonds za Live and Let Die na The Man with the Golden Gun miaka ya sabini.

Binti yake Lynn amesema: ''Alikuwa mtu mpenda watu na mwenye uwazi sana. Alipendwa sana na kila mtu.''

Aliongeza: "Sidhani alikuwa na adui hata mmoja. Kwa kweli tulibarikiwa kuwa na yeye maishani."

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages