Manukato
ya mwanamuziki huyo yamepewa jina Chibu Perfume, kwa kufuata jina lake ya utani
la Chibu Dangote.
Chupa
ya manukato hayo inauzwa takriban Sh105,000 za Tanzania.
Diamond
anaonekana kuwafuata wasanii wengine mashuhuri duniani ambao wamejiingiza
katika biashara ya manukato na hutumia umaarufu wa nembo zao kujipatia mapato
zaidi.
Wakati wa
uzinduzi huo Diamond alisema kuwa ameamua kuingia kwenye soko la kutengeneza
manukato 'Pafyum' yenye nembo yake CHIBU ili kusaidia serikali katika suala
zima la kutatua changamoto ya uhaba wa ajira nchini lakini pia kuongeza pato la
Taifa kwa kulipa Kodi.
Amesema kuwa
kuanza kutengenezwa na kuuzwa kwa pafyum hizo kutaongeza ajira kwa vijana wengi
lakini pia kutasaidia kukuza uchumi wa nchi kupitia kodi zitakazotozwa kutokana
na bidhaa hiyo ambayo wanaume na wanawake wote wanaweza kuitumia, Pafyum ya
CHIBU itapatikana katika maduka yote ya GSM na itauzwa bei ya rejareja kiasi
cha shilingi 105.000 kwa moja.
Katika
mkakati mwingine wa soko, Meneja wa Msanii huyo Bw. Salaam Mendes amesema wako
katika mazungumzo na mashirika kadhaa likiwemo shirika la ndege la Kenya Airways
kwa ajili ya kuitangaza bidhaa hiyo na kuifikisha kwenye soko la kimataifa
ikiwa ni pamoja na kuuzwa katika maduka makubwa kwenye viwanja vya ndege katika
nchi mbalimbali ambako ndege za shirika hilo zinafika
Msanii Diamond akifafanua jambo kwa Wanahabari
Manukato hayo yamepewa jina Chibu Perfume
Msanii Nasseb Abdul a.k.a Diamond Platnumz akimkabidhi
chupa ya Pafyum, mteja wake wa kwanza aliyejitambulisha kwa jina la Aisha
Azori, wakati wa uzinduzi huo.Mwana mama huyo alionekana kujisikia fahari
kununua bidhaa ambayo imetengenezwa na Msanii wa hapa nyumbani,ambae pia
anafanya vyema katika kazi zake za Muziki,kushototo ni Mmoja wa mameneja wa
Diamond Plutnamz almaarufu kwa jina la Babu Tale.
Msanii wa muziki wa kizazi kipya, ambaye amekuwa akifanya vyema
ndani na nje ya nchi (anga za Kimataifa), Naseeb Abdul a.k.a Diamond Platnumz
akizungumza mbele ya Waandishi wa habari pamoja na wadau wengine waliohudhuria
hafla fupi iliyohusu uzinduzi wa manukato (Pafyum) yake iliyoitwa CHIBU, mapema
leo jijini Dar.
Msanii Diamond akionesha moja ya Pafyum yake mbele ya
Wanahabari na wadau mbalimbali waliofika kwenye hafla hiyo fupi iliofanyika
jijini Dar Es Salaam mapema leo.
Diamond Platumz akiendelea kuzungumza na Wanahabari
pamoja na Wadau wake waliofika kulishuhudia tukio la uzinduzi huo.
Mmoja wa Meneja wa Diamond Platnumz almaarufu kwa
jina la Babu Tale akiwakaribisha wana habari na wadau mbalimbali waliofika
kushuhudia tukio hilo adhimu la uzinduzi wa Pafyum ya msanii huyo iliyojulikana
kwa jina la CHIBU.
Msanii Diamond akionesha moja ya Pafyum yake mbele ya
Wanahabari na wadau mbalimbali waliofika kwenye hafla hiyo fupi iliofanyika
jijini Dar Es Salaam mapema jana.









No comments:
Post a Comment