MITUNGI 800 ya gesi ya Kampuni ya Oryx Gas Tanzania ikiwa na makiko yake, imetolewa bure kwa wananchi wa Jimbo Morogoro Kusini Mashariki kuunga mkono juhudi za Rais Dk. Samia Suluhu Hassan kuhamasisha matumizi ya nishati safi ya kupikia.
Mitungi hiyo imetolewa kwa ushirikiano wa Kampuni ya Oryx na mbunge wa kimbo hilo Hamisi Taletale (Babu Tale) katika mkutano mkuu wa CCM Jimbo la Morogoro Kusini Mashariki mgeni rasmi akiwa Makamu Mwenyekiti wa CCM Tanzania Bara, Abdulrahman Kinana.
Akizungumza kabla ya kukabidhi mitungi hiyo Makamu Mwenyekiti wa CCM Tanzania Bara Abdulurahman Kinana amempongeza Mbunge Taletale kwa kushirikiana na wadau kugawa mitungi hiyo kwa wananchi hao kwani ni sehemu ya kuunga mkono jitihada za Rais Dk Samia Suluhu Hassan
Amesisitiza Rais Samia ameanzisha kampeni ya nishati safi yenye lengo la kumtua mzigo wa kuni mwanamke na hatimaye kumpa muda mwingi katika kufanya shughuli nyingine za kimaendeleo hasa kwa kutambua mwanamke ndio nguzo ya familia.
“Kampeni hii ya nishati safi ni matokeo ya sera na ubunifu kwa Rais Dk. Samia Suluhu Hassan. Mwaka jana alianzisha mchakato wa kuwatua akina mama mzigo wa kuni.
"Hivyo katika kufanikisha kampeni hiyo Serikali peke yake haitaweza kwasababu inahitaji fedha nyingi,hivyo nikupongeze Taletale kwa kuunga mkono jitihada za Rais katika kampeni hii,kwani tutakabidhi mitungi ya gesi kwa wananchi,lakini niwapongeze wadau wa gesi kwa kushiriki katika kufanikisha kampeni hii yenye lengo la kumtuamzigo wa kuni mwanamke,"amesema Kinana
Wakati huo huo akizungumza kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Gesi ya Oryx Tanzania, Benoite Araman, Meneja wa Mifumo ya Gesi yenye Matumizi Makubwa Oryx Gas Tanzania LTD, Richard Sawere amesema hatua ya kushirikiana na Mbunge Taletale kugawa mitungi hiyo ni hatua hiyo ni kuunga mkono jitihada za Rais Dk. Samia.
Amesema Rais Dk.Samia amedhamiria ifikapo mwaka 2030 asilimia 80 ya Watanzania wawe wananatumia nishati safi ya kupikia huku akifafanua Kampuni ya Oryx pia umeamua kunusuru uharibifu wa mazingira na kulinda afya za wananchi kwa kutumia nishati safi na rafiki kwa afya za wananchi.
"Nchini Tanzania, wananchi 33,000) wanapoteza maisha kila mwaka kwa kuvuta moshi na chembe chembe zinazotokana na mkaa na kuni. Kupika na gesi ya Oryx itatatua jambo hili," amesema.
Awali akitoa elimu kuhusu matumizi sahihi ya mitungi na majiko hayo, Meneja Masoko wa kampuni hiyo Peter Ndomba amesema sera ya kampuni hiyo ni kuhakikisha nchi nzima inatambua umuhimu wa kutumia gesi.
"Hii ni kampeni ya kitaifa ambayo Rais Samia Suluhu Hassan aliizindua kwa lengo la kuhakikisha kwamba miaka 10 ijayo zaidi ya asilimia 80 ya watanzania wawe wanatumia nishati safi".
Katika hatua nyingine Mbunge wa amesema kuwa Rais Samia ameelekeza kutekelezwa kwa kampeni ya nishati safi,hivyo Wana Morogoro Kusini Mashariki wameona Kuna kila sababu ya kumuunga mkono Rais Samia kwa vitendo kwa kutumia nishati safi ya kupikia inayotokana na gesi ili kuachana na kuni na mkaa.
No comments:
Post a Comment