Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Madini la Taifa (STAMICO) Dkt. Venance Mwasse akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi Mtendaji wa Shirikisho la wenye Viwanda Leodegar Tenga akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam.
Mwenyekiti wa DACOREMA Josephat Mkombachepa akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam.
Katibu wa Chama cha Wanawake Wachimbaji Madini Tanzania (TAWOMA) Salma Ernest akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam.
NA ABRAHAM NTAMBARA
SHIRIKA la Madini la Taifa (STAMICO) litawakutanisha wachimbaji wadogo na wadau wa madini katika mkutano wa siku mbili utakaofanyika jijini Dar es Salaam.
Akizungumza na waandishi wa habari leo Aprili 4, 2023 kuelekea mkutano huo unaotarajiwa kuanza kesho na kuhitimishwa Aprili 6, 2023 Mkurugenzi Mtendaji wa STAMICO Dkt. Venance Mwasse amesema lengo ni kutatua changamoto zinazowakabili.
Dkt. Mwasse amewataja wadau hao kuwa ni wachimbachi wadogo wa madini ya viwandani, wamiliki wa viwanda na Taasisi za kifedha.
“Tutakuwa tukikutana na wadhimbaji wa madini tofauti tofauti na sio wa madini yote. Na kesho tumeanza nawachimbaji wadogo wa madini ya viwandani,” amesema Dkt. Mwasse na kuongeza,
“Hivyo kesho ni kwa ajili ya wadau hawa watatu, ili kujua changamoto zao, kujua kwa nini tunatumia malighafi za nje, lengo pia ni kuhamasisha ujenzi wa viwanda na kuhakikisha malighafi zetu zinazalishwa kwa tija,”.
Kwamba katika mkutano huo pia umewaalika wadau wengine kama mamlaka za udhibiti kama vile Mmalaka ya Mapato Tanzania (TRA), Shirika la Viwango Tanzania (TBS) na nyingine.
Kadhalika watakuwepo wanajiolojia ambao wanahusika na upimaji wa kiwango cha upatikanaji wa madini na ubora wake.
Hivyo ametumia fursa hiyo kuwataka wachimbaji wote wadogo wa madini, wenye viwanda vya madini pamoja na wenye viwanda wanaotumia madini hayo wahudhurie kwa wingi.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Shirikisho la Wenye Viwanda (CTI), Leodegar Tenga amewasisitiza wamiliki wa viwanda ambao ni wanachama wao kuhakikisha wanatumia malighafi za ndani.
“Nisisitize nchi yetu inataka kujenga uchumi wa viwanda, hivyo linalofanyika kesho ni mwendelezo wa hiyo dhana nchini ya kujenga uchumi wa viwanda,” amesema Dkt. Mwasse.
Naye Mwenyekiti wa DACOREMA Josephat Mkombacheka amesema kuwa na Tanzania ya Madini inawezekana
No comments:
Post a Comment