A great place to access the latest news and information.

Breaking

Post Top Ad

Saturday, May 21, 2022

Rais Samia Awaapisha Viongozi Mbalimbali Ikulu Chamwino Jijini Dodoma

 

Naibu Katibu Mkuu,Dkt.Hashil Abdallah kizungumza alipokuwa akitoa hotuba ya ufunguzi wa kikao kazi cha siku mbili kati ya wahariri wa vyombo vya habari na BRELA kinahofanyika katika ukumbi wa Hoteli ya Nashera Mkoani Morogoro. 


Afisa Mtendaji Mkuu wa Brela Godfrey Nyaisa akizungumza alipokuwa akitoa salamu za utangulizi katika kikao kazi hicho cha siku mbili kinachoendelea Mkoani Morogoro.


Afisa kutoka Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Sikujua Mfaume akizungumza katika kikao kazi hicho akimuwakilisha Mkuu wa Mkoa huo Martin Shigela.



Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF) Deodatus balile akitoa neno la shukrani kwa niaba ya wahariri wa vyombo vya habari katika kikao hicho. 



Mkuu wa Kitengo cha habari na Elimu kwa Umma (BRELA) Rhoida Andusamile akizungumza alipokuwa akiongoza ratiba ya kikaokazi hicho cha siku mbili kinachofanyika Mkoani Morogoro.



Afisa Mtendaji Mkuu wa Brela Godfrey Nyaisa (kushoto) akijandiliana jambo na Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF) Deodatus balile (katikati) mara baada ya kumalizika kwa hafla ya ufunguzi wa kikao kazi hicho Mkoani Morogoro. (kulia) ni Naibu Katibu Mkuu,Dkt.Hashil Abdallah.


Naibu Katibu Mkuu,Dkt.Hashil Abdallah (wa tatu kulia aliyekaa) akiwa katika picha ya pamoja na wahariri wa vyombo vya habari mara baada ya kumalizika kwa hafla ya ufunguzi wa kikao kazi hicho Mkoani Morogoro. (Wa pili kulia) ni Afisa Mtendaji Mkuu wa BRELA Godfrey Nyaisa, na (wa kwanza kulia) ni Mwakilishi wa Mkuu wa Mkoa Sikujua Mfaume. wengine (kushoto waliokaa) ni Mjumbe wa kamati ya Utendaji Jukwaa la wahariri Tanzania (TEF) Angel Akilimali, na (wa pili kushoto) ni Mwenyekiti wa (TEF) Deodatus balile.


 
Na: Hughes Dugilo, MOROGORO.

Imeelezwa kuwa, wahariri wa vyombo vya habari nchini kwa kupitia vyombo vyao wana nafasi kubwa ya kufanikisha ukuaji wa Sekta ya Biashara nchini kwa kutoa uelewa mpana kwa wananchi kuweza kurasimisha  biashara zao.
 
Akizungumza kwa niaba ya Waziri wa Uwekezaji, Viwanda na Biashara, Dkt. Ashatu Kijaji katika kikao kazi cha siku mbili kati ya wahariri wa vyombo vya habari na BRELA kilichoanza leo Mei 21, 2022 mkoani Morogoro,  Naibu Katibu Mkuu wa wizara hiyo, Dkt. Hashil Abdallah amesema kuwa, anaamini kuwa wahariri wakijengewa uwezo juu ya majukumu ya Brela kutasaidia jamii kupata elimu hiyo.

"Kwa muktadha huu niwaombe wahariri tushirikiane kwa pamoja kwenye kufanikisha ukuaji wa sekta ya biashara nchini, hasa wananchi warasimishe biashara zao. Kupitia nyie watakuwa na uelewa wa mambo mengi,"amesema Dkt.Abdalah kwa niaba ya Waziri Dkt.Kijaji.
 
Na kuoneza kuwa,  "BRELA, muelewe kuwa wahariri wana jukumu la kuandika habari kwa usawa, pindi wanapotaka kutoa habari kwenu msiwe wagumu kutoa taarifa, kama majibu ya maswali yao yapo kwa muda huo wapewe ili umma upate taarifa kwa haraka na kama habari wanayohitaji inachukua muda kupata majibu wapewe mrejesho mapema ili waweze kusubiri ili upotoshaji usiwepo,"aliongeza.
 
Kwa upande wake Afisa Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni, (BRELA) Godfrey Nyaisa amesema kuwa, usimamiaji wa majukumu ya msingi ya BRELA umewezesha kuwa na mafanikio makubwa yenye uwazi na ukuaji wa uchumi wa Tanzania.

Aidha Nyaisa amesema kuwa, hali hiyo inatokana na uboreshaji wa mazingira ya biashara na urahisishaji wa sajili na leeni zinazotolewa na BRELA hapa nchini.

"Mafanikio haya yametokana na utekelezaji wa mikakati mikuu ya Kitaifa, Sera na Mpango wa Maendeleo ya Taifa,"amesema Bw,Nyaisa.
On Sat, May 21, 2022 at 3:55 PM Hughes Dugilo wrote:


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akimuapisha Dkt. Charles Enock Msonde kuwa Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za MtaaTAMISEMI(Elimu) katika hafla fupi iliyofanyika Ikulu Chamwino Jijini Dodoma tarehe 21 Mei,2022.



Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akimuapisha Dkt. Maduhu Isaac Kazi kuwa Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi katika hafla fupi iliyofanyika Ikulu Chamwino Jijini Dodoma tarehe 21 Mei,2022.



Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akimuapisha Balozi John Michael Haule kuwa Kamishna wa Tume ya Utumishi wa Umma katika hafla fupi iliyofanyika Ikulu Chamwino Jijini Dodoma tarehe 21 Mei,2022.




Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akimuapisha Immaculata Peter Ngwalle kuwa Kamishna wa Tume ya Utumishi wa Umma katika hafla fupi iliyofanyika Ikulu Chamwino Jijini Dodoma tarehe 21 Mei,2022.


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akimuapisha Khadija Ali Mohamed Mbarak kuwa Kamishna wa Tume ya Utumishi wa Umma katika hafla fupi iliyofanyika Ikulu Chamwino Jijini Dodoma tarehe 21 Mei,2022.

 

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akimuapisha Susan Paul Mlawi kuwa Kamishna wa Tume ya Utumishi wa Umma katika hafla fupi iliyofanyika Ikulu Chamwino Jijini Dodoma tarehe 21 Mei,2022.




Viongozi mbalimbali walioapishwa Wakila Kiapo cha Maadili kwa Viongozi wa Umma katika hafla iliyofanyika Ikulu Chamwino Mkoani Dodoma.


Spika wa Bunge Dkt. Tulia Ackson akiwa na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (Menejimenti ya Utumishi wa Umma na utawala Bora) Jenista Mhagama, Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa TAMISEMI Innocent Bashungwa, Waziri wa mambo ya Ndani ya Nchi Hamadi Masauni pamoja na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Hussein Katanga wakiwa katika hafla fupi ya Uapisho wa Viongozi mbalimbali tarehe 21 Mei 2022 Ikulu Chamwino Jijini Dodoma.



Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Viongozi mbalimbali mara baada ya tukio la Uapisho lililofanyika Ikulu Chamwino Jijini Dodoma tarehe 21 Mei, 2022.



Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa katika picha ya pamoja na Viongozi mbalimbali aliowaapisha Ikulu Chamwino Mkoani Dodoma tarehe 21 Mei, 2022.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Pages