JUMLA ya Wanawake 9000 nchini wameweza kuchunguzwa Saratani ya Shingo ya Kizazi na wanawake 550 wamegundulika na kupatiwa matibabu ya ugonjwa huo.
Hilo limewekwa wazi na Mkurugenzi wa Benki ya Taifa ya Biashara (NBC) Theobald Sabi wakati wa uzinduzi wa Mbio za NBC Dodoma Marathon zitakazofanyika kwa msimu wa tatu mwaka 2022.
Sabi amesema, Katika kuunga mkono juhudi za mapambano ya kansa ya kizazi kwa Wanawake ' Benki ya NBC imeandaa Marathon iitwayo 'NBC Dodoma Marathon' yenye lengo la kusaidia Wanawake zaidi ya 20,000 wenye kansa ya kizazi.
Akizungumza wakati wa uzinduzi wa marathon hiyo ambayo itafanyika Dodoma Julai 31, 2022, Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NBC, Sabi amesema kwa Tanzania pekee ndani ya mwaka Wanawake zaidi ya 1000 wanaopimwa wanakutwa na saratani ya kizazi.
Amesema, ndani ya miaka miwili wameweza kushirikiana na Hospitali ya Saratani ya Ocean Road na wamefanikiwa kuwachunguza wanawake 9000 na wanawake 550 wakigundulika kuwa na ugonjwa huo na wameweza kupatiwa matibabu na wamepona.
"Cancer ya Wanawake ni cancer inayoongoza kuua Wanawake wengi zaidi katika nchi zinazoendelea mfano Tanzania kwa mwaka Wanawake 1400 wanaopimwa wanakutwa na saratani ya kizazi na katika hao 1400 zaidi ya asilimia 30 wanapoteza maisha katika miaka mitatu kwasababu wanakosa tiba zinazostahili"
Aidha Sabi amesema katika harakati za kupambana na kansa ya kizazi kupitia marathon hiyo, Wana lengo la kupata milioni 200 kwa mwaka huu na katika miaka miwili iliyopita walikusanya jumla ya milioni 300 ambapo fedha zote hizo watazipeleka katika hospitali ya Ocean Road kwaajili ya matibabu ya Wanawake hao wenye kansa ya kizazi;
"Cancer hii inatibika hivyo sisi kazi yetu ni kufanya Kampeni ya kukusanya pesa, kufanya awareness na lengo letu ni kupata milioni 200 mwaka huu ambazo zitasaidia kuwapa ocean road na kutibu"
Sabi amesema Muitikio wa watu kushiriki kwenye marathon ni mkubwa ambapo kwa miaka miwili wameshapata zaidi ya watu 4000, na mwaka huu wanategemea kupata zaidi ya watu 5000.
Aidha, Sabi Lengo ni kutengeneza ufahamu kwamba cancer hii inatibika Wanawake wawe na tabia ya kupima angalau Kila mwaka wakina mama wawe wanajua Afya zao.
Kwa upande wa Mkurugenzi wa Hospitali ya Saratani ya Ocean Road Dkt Julius Kaisalage amesema wanaishukuru Benki ya NBC wa jambo kubwa wanalolifanya la kuhakikisha wanasaidiana na taasisi yao katika kupambana na ugonjwa wa saratani ya shingo ya kizazi.
"Tunapenda kuwashukuru NBC na ukiachilia mbali wanatuunga mkono katika kuwapatia matibabu wanawake na katika miaka miwili tumeshirikiana kwa ukaribu mkubwa sana na wanawake 9000 wameweza kuchunguzwa na wengine 550 wamepatiwa matibabu na wamepona,"
"Ugonjwa huu unaanzia pindi msichana anapoanza kushiriki tendo la kujaamini na Uchunguzi wa saratani ya shingo unafanyika kwa mabinti wa kuanzia miaka 14 na kuendelea na bado tunaendelea kutoa elimu kuwa ugonjwa huu unatibika na unapona kikubwa wasiache kufanyiwa uchunguzi,"ameongeza.
NBC Dodoma Marathon imesajiliwa kimataifa ambapo wana cheti kinachotambulika na wamekuwa wakishirikisha wakimbiaji wa kimataifa kutoka ndani na nje ya nchi.
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Taifa ya Biashara (NBC) Theobald Sabi (katikati) akiwa pamoja na Mkurugenzi wa Taasisi ya Saratani Ocean Road Dkt Julius Kaisalage (wa pili kushoto), Rais wa chama cha riadha Tanzania Silas Isangi (kushoto),Mkurugenzi wa Uendeshaji EFM na TVE Denis Ssebo wakati wa uzinduzi wa NBC Dodoma Marathon kwa msimu wa tatu inayotarajiwa kufanyika Julai 31 mwaka huu Jijini Dodoma.
No comments:
Post a Comment