Bodi
ya Wataalamu wa Ununuzi na Ugavi (PSPTB) imetoa mafunzo kwa Wanafunzi wa Taasisi ya Uhasibu Tanzania (TIA) wa Astashada, Stashada na Shahada
zinazochukua kozi za Ununuzi na Ugavi.
Akizungumza
mara baada ya mafunzo hayo, Kaimu Mkurugenzi wa mafunzo wa Bodi ya
wataalumu wa Ununuzi na Ugavi (PSPTB), Amani Ngonyani amesema Bodi hiyo
imeendelea kuwapa mafunzo Wanafunzi wa Vyuo mbalimbali wanaochukua kozi
ya Ununuzi na Ugavi kuhusu shughuli zinazofanywa na Bodi hiyo, Mitahani
inayotungwa na Bodi, Usajili kwa njia ya mtandao na masuala ya ajira
pamoja na maadili na miiko ya Taaluma hiyo.
Ngonyani
amesema Wanafunzi hao wamekuwa na mwamko wa kiudhiria mafunzo hayo
zaidi katika kuongeza dhamani kwenye taaluma ya Ununuzi na Ugavi hasa
pale unapofanya mitihani ya Bodi na pia wakati wa unapesa cheti cha
CPSP anapata cheti cha IFPSM.
Naye Kaimu
Mkurugenzi wa Maendeleo ya Taaluma wa PSPTB Amos Kazinza amesema
Taaluma ya Ununuzi inabidi kusimamiwa ipasavyo ili kuweza kuondoa mifumo
ya urasimu kwenye Ununuzi wa umma.
Pia amewataka Wanafunzi
wa Chuo cha Uhasibu Tanzania (TIA) wa Astashada, Stashada na Shahada
zinazochukua kozi za Ununuzi na Ugavi kuweza kusoma kwa bidii ili
kuendana na soko la ajira hasa kufanya mitihani ya Bodi.
"Nawaomba
mkimaliza masomo ni vizuri mkajisajili kwenye Bodi pamoja na kufanya
mitihani ya Bodi ili kutambulika kwani huwezi kufanya kazi za Ununuzi na
Ugavi bila kutambulika na Bodi hiyo" alisema Kazinza
Kaimu
Mkurugenzi wa Maendeleo ya Taaluma wa PSPTB Amos Kazinza akitoa mada
kuhusu Sheria na maadili ya Taaluma ya Ununuzi wakati wa kutoa elimu kwa
wanafunzi wa Astashada, Stashada na Shahada wanaosoma masomo ya Ununuzi
katika Taasisi ya Uhasibu Tanzania (TIA) iliyopo Dar es Salaam ikiwa na
lengo la kutoa elimu kuhusu kazi zinazofanywa na Bodi hiyo.
Kaimu
Mkurugenzi wa mafunzo wa Bodi ya wataalumu wa Ununuzi na Ugavi
(PSPTB) , Amani Ngonyani akitoa mada kuhusu namna ya kuongeza dhamani
kwenye taaluma ya Ununuzi na Ugavi wakati wa kutoa elimu kwa wanafunzi
wa Astashada, Stashada na Shahada wanaosoma masomo ya Ununuzi katika
Taasisi ya Uhasibu Tanzania (TIA) iliyopo Dar es Salaam ikiwa na lengo
la kutoa elimu kuhusu kazi zinazofanywa na Bodi hiyo.
Mhadhiri
wa Masomo ya Ununuzi wa Chuo cha Uhasibu Tanzania (TIA) Ibrahim Uswege
akizungumza jambo wakati wa kutoa elimu kwa wanafunzi wa Astashada,
Stashada na Shahada wanaosoma masomo ya Ununuzi katika Taasisi ya
Uhasibu Tanzania (TIA) iliyopo Dar es Salaam ikiwa na lengo la kutoa
elimu kuhusu kazi zinazofanywa na Bodi hiyo.
Meneja
Masoko na Uhusiano kwa Umma ( PSPTB), Shamim Mdee akitoa maelezo kuhusu
kazi zinazofanywa na Bodi hiyo wakati wa kutoa elimu kwa wanafunzi wa
Astashada, Stashada na Shahada wanaosoma masomo ya Ununuzi katika
Taasisi ya Uhasibu Tanzania (TIA) iliyopo Dar es Salaam ikiwa na lengo
la kutoa elimu kuhusu kazi zinazofanywa na Bodi hiyo.
Meneja
Tehama wa wa Bodi ya Wataalumu wa Ununuzi na Ugavi (PSPTB) Grace Mselle
akitoa mada kuhusu namna ya mwanafunzi anavyoweza kujisajili pamoja na
kufanya mitihani ya Bodi wakati wa kutoa elimu kwa wanafunzi wa
Astashada, Stashada na Shahada wanaosoma masomo ya Ununuzi katika
Taasisi ya Uhasibu Tanzania (TIA) iliyopo Dar es Salaam ikiwa na lengo
la kutoa elimu kuhusu kazi zinazofanywa na Bodi hiyo.
No comments:
Post a Comment