
Filamu ya “Royal Tour”
ambayo imezinduliwa siku ya jumatatu ya tarehe 18 April, 202 inatoa
fursa za ukuaji wa uchumi kwa Tanzania, hayo amesema Mkurugenzi Mtendaji
wa Benki ya CRDB, huku akibainisha namna ambavyo benki hiyo imejipanga
katika kuwawezesha Watanzania kunufaika na fursa zitakazotokana na
filamu hiyo.
Nsekela
akiwa ni miongoni mwa ujumbe wa Jumuiya ya Mabenki Tanzania (TBA) ambao
wameambatana na Rais Samia katika safari yake ya Marekani, alisema
Royal Tour itaongeza kwa kiasi kikubwa ujio wa watalii na uwekezaji
nchini.
“Tunatarajia
The Royal Tour itafikia malengo yake ya kuitangaza Tanzania kama nchi
inayoongoza kwa vivutio vya utalii duniani na hivyo kusaidia kuvutia
watalii kuja Tanzania…Pia itakuza biashara kati ya Tanzania na nchi
nyingine na kuvutia wawekezaji kuja kuwekeza nchini,” alisema.
Wakiwa kwenye ziara ya uzinduzi wa “The Royal Tour”,
ujumbe wa Benki ya CRDB ulikutana na Citibank, pamoja na Shirika la
Pegasus, ambapo walijadili masuala ya biashara ambayo yanaweza
kuinufaisha Tanzania na Watanzania.
Ujumbe
wa Benki ya CRDB ukiongozwa na Mkurugenzi Mtendaji, Abdulmajid Nsekela
(wa pili kulia) wakiwa katika picha ya pamoja na Mkurugenzi Mtendaji wa
Moody's Investors Service Ana Arsov (katikati) walipotembelea Makao
Makuu ya Moody's yaliyopo katika Jiji la New York Marekani. Wengine
pichani ni Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Benki ya CRDB, Tully Mwambapa
(wa pili kushoto), Meneja Mwandamizi wa Uwekezaji Endelevu wa Benki
hiyo, Kenneth Kasigila (wa kwanza kushoto), na Afisa Uhusiano wa
Biashara, Iman Tassama.
Ujumbe
wa Benki ya CRDB pia uliitembelea Moody's na kufanya majadiliano ya
hali ya juu kulingana na msimamo wa soko, ikijumuisha kuwajengea uwezo,
kupata taarifa na ufuatiliaji wa viwango vya mikopo.
Mkutano
na watendaji wakuu wa Citibank ulijadili vipaumbele muhimu vya pamoja
ikiwamo kusaidia uwezeshaji wa kiuchumi kwa wajasiriamali wadogo na
wakati, kwa kuzingatia uwezeshaji wa wanawake na vijana, uwekezeaji
katika huduma za kidijitali, na kusaidia ajenda ya Uchumi wa Bluu.
"Tulijadili
pia msaada wa kiufundi kwa Benki ya CRDB ili kuimarisha uwezo wa Benki
katika kuhudumia kundi la wajasiriamali ambao kwa kiasi kukubwa
wameathirika na janga la COVID19 na kukidhi mahitaji yanayokua kwa kasi,”
alisema Nsekela huku akibainisha kuwa katika mkutano huo walijadili
ushirikiano wa kibiashara katika kampuni tanzu ya nchini Jamhuri ya
Kidemokrasia ya Kongo (DRC) inayotarajiwa kuzinduliwa hivi karibuni.
Katika
kikao na watendaji kutoka Pegasus, kampuni ya Kimarekani inayowekeza
kwenye biashara zinazozingatia utunzaji wa mazingira na zinazohusiana na
afya, kampuni hiyo ilieleza nia yake ya kuingia katika soko la Tanzania
na kujadilijinsi gani inaweza kushirikiana na Benki ya CRDB.

Filamu
ya Royal Tour ambayo ilirekodiwa nchini Tanzania - itatumika kutangaza
vivutio vya utalii vya nchi kwa kiwango cha kimataifa, ikiwa ni sehemu
ya mkakati mpya wa serikali za kukuza utalii baada ya janga la kimataifa
la Covid-19. Baada ya kuzinduliwa kwa mara ya kwanza huko New York
Aprili 18, filamu hiyo pia itazinduliwa mjini Los Angeles Aprili 21, Dar
es Salaam Aprili 28, na baadaye Zanzibar.
Rais
Samia alihusika katika kurekodi filamu hiyo mwaka jana alipokuwa
akisafiri katika maeneo mbalimbali ya vivutio vya utalii akiwa na na
mwandishi wa habari nguli aliyeshinda tuzo ya Emmy, Peter Greenberg.
Sekta
ya utalii ya Tanzania ambayo iliathiriwa vibaya na janga la Covid-19,
imekuwa katika hali ya ahueni, ambapo takwimu za Benki Kuu ya Tanzania
zinaonyesha kuwa katika kipindi cha mwaka unaoishia Februari 2022,
mapato ya fedha za kigeni kutoka sekta hiyo yaliongezeka hadi dola za
kimarekani bilioni 1.457 kutoka dola za kimarekani bilioni 645.4 katika
kipindi kama hicho mwaka jana. Ongezeko hilo lilitokana na ongezeko la
asilimia 87.9 la watalii waliofika na kufikia wasafiri 958,173 katika
kipindi kinachoishia Februari 2022.
Kwa
mujibu wa Nsekela, filamu ya Royal Tour - ambalo Mhariri wa Wasafiri wa
Habari wa CBS Peter Greenberg ametayarisha - itasaidia kuuelezea
ulimwengu utajiri wa maliasili nyingi za Tanzania, ikiwa ni pamoja na
rasilimali, utamaduni, mila na desturi za Taifa letu la Tanzania.
Ujumbe
wa Benki ya CRDB ukiongozwa na Mkurugenzi Mtendaji, Abdulmajid Nsekela
(wa nne kulia) wakiwa katika picha ya pamoja na Viongozi Waandamizi wa
Citibank walipotembelea Makao Makuu ya Citibank jijini New York. Nsekela
aliongozana na Mkurugenzi wa Mawasiliano, Tully Mwambapa (wa pili
kushoto), Meneja Mwandamizi wa Uwekezaji Endelevu wa Benki hiyo, Kenneth
Kasigila (wa kwanza kushoto), na Afisa Uhusiano wa Biashara, Iman
Tassama.
"Tuna
madini ya Tanzanite yanayopatikana Tanzania pekee duniani kote...tuna
hifadhi kubwa ya gesi asilia, makaa ya mawe, mito, maziwa, bahari na
mapori ya akiba. Tuna zaidi ya makabila 100 ambayo yanaishi kwa amani.
Tuna utamaduni tajiri na mila, vyakula asilia, historia na mavazi yetu.
Haya yote yanaunda fursa ya kiuchumi," alisema.
Nsekela
alidokeza kuwa Benki ya CRDB imejipanga vyema kunaweka mazingira
wezeshi yatakayosaidia wananchi na Taifa kunufaika na fursa zitokanazo
na filamu ya Royal Tour, kupitia huduma na bidhaa bunifu zinazotolewa na
benki hiyo.
Baadhi
ya huduma na bidhaa za Benki ya CRDB zitakazowezesha kusaidia wateja
kunufaika na fursa hizo ni pamoja na huduma za uwezeshaji kupitia mikopo
ya Uwekezaji na uendeshaji wa biashara, pamoja na mifumo thabiti ya
malipo kupitia vifaa vya manunuzi (PoS), huduma za TemboCard, pamoja na
mifumo ya malipo ya kidijitali
No comments:
Post a Comment