Waziri wa Maendeleo ya Jinsia Wanawake na Makundi Maalum Dkt. Doroth Gwajima akizungumza wakati alipokuwa
mgeni rasmi kwenye hafla ya Usiku wa Mwanamke wa Pwani iliyowakutanisha
wanawake wa Mkoa wa Wilaya zote za Mkoa wa Pwani kwenye Ukumbi wa
Destiny uliopo maeneo ya Kwa Marias Kibaha.
Mkuu wa Mkoa wa Pwani Alhaji Abubakari Kunenge akizungumza wakat
hafla ya Usiku wa Mwanamke wa Pwani iliyowakutanisha wanawake wa Mkoa
wa Wilaya zote za Mkoa wa Pwani kwenye Ukumbi wa Destiny uliopo maeneo
ya Kwa Marias Kibaha.
Na Khadija Kalili, Kibaha
WAZIRI
wa Maendeleo ya Jinsia Wanawake na Makundi Maalum Dkt. Doroth Gwajima
amesema kuwa kutokana na Mkoa wa Pwani kutia fora kwa kuwa na mwamko wa
kuwa na majukwaa imara ya wanawake atamuomba wakati wa kuzindua rasmi
aje kuzindua Kitaifa Mkoani Pwani.
Waziri
Gwajima alisema hayo alipokuwa mgeni rasmi kwenye hafla ya Usiku wa
Mwanamke wa Pwani iliyowakutanisha wanawake wa Mkoa wa Wilaya zote za
Mkoa wa Pwani kwenye Ukumbi wa Destiny uliopo maeneo ya Kwa Marias
Kibaha.
Aidha
amewataka wanawake katika Mimoa mingine kuiga mfano wa mwamko
ulioonyeshwa na na majukwaa ya Wanawake wa Mkoa wa Pwani kwa kujiunga
na majukwaa ya uwezeshaji wanawake kiuchumi huku akisisitiza kuwa
wanawake wote wanapaswa kujiunga kwa kuanzia katika ngazi ya kata kwa
sababu yatawasaidia kuwainua kiuchumi kuanzia chini.
Usiku
huo wa Mwanamke wa Pwani ambayo uliandaliwa na Ofisi ya Mkuu wa na
Mkoa wa Pwanj na kusimamiwa na Katibu Tawala wa Mkoa wa Pwani Mhandisi
Mwanasha Tumbo kwa kushirikiana na Mkuu wa Wilaya ya Kibaha Sara
Msafiri.
"Pwani
ninyi ni kinara wa agenda hii ya uanzishwaji wa majukwaa ya Wanawake
huku lengo kubwa likiwa kumuwezesha mwanamke kiuchumi hivyo nawapongeza
sana hasa mnavyoongelea kufungua Kiwanda chenu hili siyo jambo dogo
hivyo kabla ya mwezi wa tatu haujaisha mimi nitakuja Pwani kuwatembelea
Ili tuweze kujadiliana namna ya kuweza kuupaisha zaidi Mkoa wenu"
alisema Dkt. Gwajima.
"Wanawake
wote wa Mikoa mingine wanatakiwa wajiunge na majukwaa ya wanawake Ili
waweze kupata mikopo ambayo itawawezesha kiuchumi, ila kwa wale ambao
hawajajiunga na majukwaa haya wanatuchelewesha lakini hawatoweza
ninachosema hapa ni kwamba wapewe hamasa zaidi Ili waweze kujiunga na
majukwaa hayo Ili waweze kuvuka hapo walipo"alisema Gwajima.
Gwajima
alisema kuwa mabaraza hayo ambayo kwa sasa yako katika ngazi ya Wilaya,
Mkoa na Taifa huku ngazi ya Kata yakiwa hayana nguvu sana yamefanya
vizuri ambapo wanawake waneweza kujiinua kiuchumi.
"Tumpongeze
Rais wetu wa awamu ya sita Samia Suluhu Hassan kwa wa kuyawezesha kwa
kuwapatia fedha za mikopo ambapo yameleta mabadiliko makubwa kiuchumi
kwa wanawake ifike wakati sasa yaanzie ngazi ya kata," alisema Gwajima.
" Pwani ya sasa siyo ya kucheza ngoma na mdundiko ya sasa imebadilika haya ndiyo mawazo tunayoyataka,"alisema Gwajima.
Kwa
upande wake Mkuu wa Mkoa wa Pwani Alhaji Abubakari Kunenge alisema kuwa
Rais Samia ameonyesha uwezo wa mwanamke katika ukombozi kwao hivyo
anampongeza sana ambapo anatimiza mwaka mmoja tangu alipoingia
madarakani mwezi Machi mwaka jana.
Kunenge
alisema kuwa kwa sasa watoto wa kike wa Mkoa wa Pwani wanapata elimu na
hata kama wakichezwa ngoma hawapewei mume wanapewa elimu hio ni jambo
la kuwapa pongezi huku akisisitiza kuwa mila na desturi ni muhimu
lakini elimu ni muhimu zaidi.
Naye
mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake wa Tanzania (UWT) Mkoa wa Pwani Farida
Mgomi alisema kuwa wanawake wamenufaika sana na wanakila sababu ya
kumshukuru Rais kwa kazi kubwa anayoifanya.
Mgomi
alisema kuwa wao kama viongozi wa chama serikali watamuunga mkono kwa
kumkwamua mwanamke kiuchumi na kuhamasisha kujiunga na majukwaa hayo ya
kiuchumi ili kila mwanamke uchumi wake
No comments:
Post a Comment