ZAIDI
ya shilingi Trilioni 25 zinatarajiwa kutumika kwa ajili ya ujenzi wa
reli ya kisasa (SGR) kwa vipande vya Dar es Salaam Kigoma na Dar es
Salaam pamoja Mwanza
Akizungumza
na waandishi habari Mkurugenzi Mkuu Shirika la Reli Tanzania (TRC)
Masanja Kadogosa wakati Kamati ya Bunge ya Bajeti ilipotembelea mradi
wa reli ya kisasa toka stesheni hadi Soga mkoani Pwani.
Kadogosa
amesema ujenzi huo unatumia fedha za ndani pamoja na mikopo mbalimbali
kutoka taasisi za fedha na kwamba Sh bilioni 600 imeshatolewa kwa
mkandarasi kwa ajili ya ujenzi wa kipande cha Makutupora Dodoma hadi
Tabora.
Amesema
ujenzi wa reli kipande cha Dar es Salaam hadi Morogoro ulitumia fedha
za ndani na mikopo mbalimbali kutoka Denmark na Sweden ambayo ilikuwa na
riba ya asilimia tatu ambapo ni mkopo nafuu na ulipaji ni muda mrefu.
"Mkopo
huu ni wa miaka 20 na zaidi na ni mkopo mzuri sana kwani ulitupa fursa
ya kufanya majadiliano. Upembuzi yakinifu kuhusu mradi huu ulifanywa na
serikali ya awamu ya nne na serikali nyingine zimeendeleza," alisema
Kadogosa.
Alisema
katika mradi huo hawatategemea mizigo pekee kujiendesha badala yake
itashirikisha sekta binafsi kwa ajili ya kuanzisha huduma za kifedha,
migahawa na biashara ambazo zitawaongezea mapato.
"Ni
lazima reli ijiendeshe kwa kutumia mapato mbalimbali yatakayokusanywa
kutoka katika vitega uchumi tulivyoviweka kwenye vituo vyetu vyote vya
abiria," alisisitiza.
Alisema
wakikamilisha ujenzi huo kwa kuunganisha maeneo muhimu ya bandari
itachukua miaka 15 kupata faida na kwamba wanafanya jitihada mbalimbali
kurudisha mzigo mkubwa unaochukuliwa Uganda kuliko nchi zote.
Kwa
upande wake, Mwenyekiti wa kamati hiyo, Daniel Sillo alisema serikali
imefanya kazi kubwa katika mradi huo wa Kilometa 300 na kwamba asilimia
kubwa imekamilika (95.3).
Alisema
reli ni muhimu kwa uchumi na kijamii na kwamba ni mradi muhimu kwa
maendeleo ya nchi hivyo, wanaamini wataishauri vyema serikali katika
utendaji kazi.
Naye,
Naibu Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Atupele Mwakibete alisema tayari Sh
trilioni 14.5 zimeshalipwa kwa mkandarasi na kwamba Sh trilioni saba
niza mikataba mbalimbali hivyo, wanaamini katika bajeti ijayo
itawasaidia kutekeleza miradi kwa wakati ili kutoa huduma bora kwa
jamii.
Alisema
wameagiza behewa 44 na vichwa vipya vitatu kwa ajili ya kupeleka mizigo
katika bandari ya Isaka na kwamba wanatarajia kufanya mazungumzo na
wafanyabiashara wa nchi za Rwanda, Congo, Burundi na Uganda ili kutumia
fursa hiyo.
No comments:
Post a Comment