Afisa
Elimu Huduma na Elimu kwa Mlipa Kodi (TRA) Mkoa wa Tanga Salim Bakar
akizungumza wakati akifungua mafunzo maalumu kwa wafanyabiashara Jijini
Tanga waliosajiliwa na kodi ya ongezeko la Thamani (VAT).
Afisa
Elimu Huduma na Elimu kwa Mlipa Kodi (TRA) Mkoa wa Tanga Salim Bakar
akizungumza wakati akifungua mafunzo maalumu kwa wafanyabiashara Jijini
Tanga waliosajiliwa na kodi ya ongezeko la Thamani (VAT).
MMOJA wa wafanyabiashara walioshiriki mafunzo hayo akizungumza na waandishi wa habari ambapo alipongeza mfumo huo mpya
Sehemu ya wafanyabiashara wakifuatilia mafunzo hayo
Sehemu ya wafanyabiashara wakifuatilia mafunzo hayo
NA OSCAR ASSENGA, TANGA
MAMLAKA ya Mapato Tanzania (TRA) Mkoa wa Tanga wametoa mafunzo maalumu
kwa wafanyabiashara Jijini waliosajiliwa na kodi ya Ongezeko la Thamani
(VAT) kuhusu mfumo mpya ulioboreshwa wa uwasilishaji wa Ritani ya Kodi
la Ongezeko la Thamani (VAT).
Akizungumza wakati akifungua
mafunzo hayo Afisa Elimu Huduma na Elimu kwa Mlipa Kodi (TRA) Mkoa wa
Tanga Salim Bakar wakati wa mafunzo maalumu kwa wafanyabiashara Jijini
Tanga waliosajiliwa na kodi ya ongezeko la Thamani (VAT).
Alisema
mafunzo hayo yanakuwa endelevu kwa wilaya nyengine kuhusiana mfumo mpya
ulioboreshwa wa uwasilishaji wa ritani za kodi la ongezeko la thamani
(VAT) kwa walipa kodi pindi yanapojitokeza mabadiliko, marekebisho ya
sheria za kodi lengo ni kukuza uelewa wa wafanyabiashara wanapotumia
mifumo kuwasilisha ritanio za kodi.
Alisema mamlaka hiyo
imeanzisha mfumo wa uwasilishaji wa Ritani ulioboreshwa na ilitoa
Taarifa mwezi February mwaka huu na kwamba kuanzia ritani za mwezi Machi
za VAT ambazo zinawasilishwa mwezi Aprili walipa kodi watapaswa kutumia
mfumo mpya ulioboreshwa wa uwasilishaji wa ritani.
Afisa huyo
alisema mfumo huo utakuwa na faida nyingi ikiwemo urahisi kwa mtumiaji
ambapo mlipakodi atahitajika kutumia akaunti moja ya uwasilishaji wa
ritani tofauti na awali ilikuwa ikimlazimu mlipakodi kutumia tofauti
kulingana na aina ya ritani ya kodi.
Aidha alisema faida
nyengine ni ujazaji wa ritani umerahisishwa ambapo taarifa za manunuzu
katika ritani ya VAT zitaingizwa kwa kutumia namba ya uthibitisho
(Verfication Code) tu iliyopo katika risiti ya kieletroniki tofauti na
awali ambapo itamlazimu mlipakodi kujaza taarifa za kadhaa kama Jina la
Muuzaji, Namba ya Usajili wa VAT, Namba na tarehe risiti/ankra, Kiasi
cha Manunuzi na VAT katika manunuzi husika.
“Kwa kweli mfumo
huo mpya utaongeza mapato ya serikali na lengo la serikali ni
kumrahisishia mlipakodi atape huduma iliyoboreshwa bila kufika TRA na
hivyo atapata kuwasilisha ritani akiwa ofisini au nyumbani bila kufika
TRA”Alisema
Hata hivyo alisema mfumo huo utawezesha kufanyika
kwa marekebisho ya kodi pale yanapotokea kama yalivyoanishwa katika
sheria ya kodi la ongezeko la thamani sura ya 148 tofauti na utaratibu
wa sasa ambapo mlipakodi alihitajika kuandika barua ya kutoa taarifa kwa
Kamisha.
Awali akizungumza mmoja wa wafanyabiashara hao kutoka
SD Supermarket Moniraju Vasant alisema wanashukuru kupatiwa elimu hiyo
ya mabadiliko hayo na kwamba mpango huo utakuwa ni mzuri kwa ajili ya
kuboresha mapato TRA.
Alisema pia utawapunguzia usumbufu wa
kwenda TRA kupata huduma badala yake kutumia mifumo hiyo wakiwa ofisini
kwao na hivyo kuwawezesha kutekeleza majukumu mengine
Post Top Ad
Your Ad Spot
Monday, March 7, 2022
Home
BIASHARA
TRA TANGA YATOA MAFUNZO KWA WAFANYABIASHARA KUHUSU MFUMO MPYA ULIOBORESHWA WA UWASILISHAJI WA RITANI ZA VAT
TRA TANGA YATOA MAFUNZO KWA WAFANYABIASHARA KUHUSU MFUMO MPYA ULIOBORESHWA WA UWASILISHAJI WA RITANI ZA VAT
Tags
BIASHARA#
Share This
About kilole mzee
BIASHARA
Labels:
BIASHARA
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Post Top Ad
Your Ad Spot
No comments:
Post a Comment