A great place to access the latest news and information.

Breaking

Post Top Ad

Your Ad Spot

Tuesday, March 8, 2022

STAMICO YAFUNIKA MAADHIMISHO SIKU YA MWANAMKE




Stamico wafunika maadhimisho siku ya mwanamke uwanja wa Uhuru


WAFANYAKAZI Serikali na Taasisi zisizo za kiserikali wanawake katika Mkoa wa Dar es Salaam wameungana katika maadhimisho ya siku ya wanawake duniani ambayo hufanyika kila mwaka Machi 8 kwa kuwa kauli mbiu ya Kizazi cha Haki na Usawa kwa Maendeleo Endelevu.



Katika Maadhimisho hayo wanawake wamesema kuwa kuadhimisha huko ni kuonyesha safari ya mwanamke na kuangalia mafanikio.

Hata hivyo katika maadhimisho haya wanawake wamejitokeza kwa shamlashamla ambazo zinaonyesha maendeleo endelevu yanaonekana.




Wafanyakazi wa Wanawake Shirika la Taifa la Madini (Stamico) wakiwa katika maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani ambayo hufanyika kila Machi 8 ambapo wanawake hao wameonyesha kujiamini katika kutenda kazi kwa maendeleo ya Taifa kama kauli mbiu ya Siku ya Wanawake Duniani Kizazi cha Haki na Usawa katika Maendeleo Endelevu,wafanyakazi hao walikuwa na shamlashala za za namna yake katika katika viwanja vya uhuru jijini Dar es Salaam.


Mmoja ya wafanyakazi wanawake walipotembelea kiwanda chakutengenezea mkaa wa mawe kilichopo msasani jijini Dar es Salaam Latifa Abdallah akiuliza swali kwa Mhandisi Happy Mbenyange wakati walipotembelea kiwanda hicho wakiadhimisha siku ya wanawake Duniani yaliyohitimishwa leo,



Mhandisi wa Shirika la Madini la Taifa (STAMICO) Happy Mbenyange (kushoto), akitoa maelekezo kwa baadhi ya wafanyakazi wanawake wa Shirika la hilo walipotembelea kiwanda chakutengenezea mkaa wa mawe rafiki kwa mazingira kilichopo msasani jijini Dar es Salaam wakati wa maadhimisho ya siku ya wanawake Duniani yaliyohitimishwa leo duniani kote




Na Stella  Kessy

KATIKA Maadhimisho ya  Siku ya Wanawake Duniani   Shirika la Madini la Taifa (STAMICO) limetoa pongezi kwa serikali ya awamu ya Sita kwa jitihada za kuwawezesha Wanawake katika sekta mbalimbali.

Kauli hiyo imetolewa leo na Mhandisi wa (STAMICO) Pili Athumani  amesema katika shirika la madini limezingatia hilo kwa kuwapa kipaumbele  mwanawake  na kutoa majukumu sawa na wanaume ili kutekeleza kauli mbiu ya Siku ya wanawake.

"Kampuni yetu inathamini sana wanawake,kwani kwa kulingana na kauli mbiu ya mwaka huu ni  'kizazi cha haki na usawa  kwa maendeleo endelevu kwa jamii' katika sekta ya madini suala hili limepewa kipaumbele, kwani wanawake wamekuwa wanapewa kipaumbele katika kusimamia miradi"Amesema.

Ameongeza kuwa katika sekta ya madini mwitiko wa wanawake umekuwa mwingi  katika shughuli zote za madini Wanawake wengi wamekuwa wakijitokeza na kujiari na wanazitumikia fursa kama ifuatavyo.

"katika shirika letu la madini sisi Kama wanawake waandisi tumekuwa tukipewa majukumu kama wanaume kwahiyo wanaitekeleza hiyo kauli mbiu  ipasavyo kwani tunaopewa miradi mingi ambayo tunasimami na kutendea haki kadri ya uwezo wetu na kuifanikisha na kutoa matokeo chanya"

Pia ametoa wito kwa serika endelee kutuamini sisi wanawake kwa kupewa majukumu mbalimbali kwani wanawake tunaweza.


No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages