A great place to access the latest news and information.

Breaking

Post Top Ad

Your Ad Spot

Sunday, March 6, 2022

TANZANIA COMMERCIAL BANK YAMFURAHISHA RAIS MWINYI KONGAMANO LA WANAWAKE ZANZIBAR

 



Mke wa Rais wa Zanzibar Mama Mariam Mwinyi ambae pia ni Mwenyekiti wa Taasisi ya Zanzibar Maisha Bora Foundation (ZMBF) na (wa pili kushoto), akipokea hundi ya shilingi milioni kumi kutoka kwa Afisa Mtendaji Mkuu wa Tanzania Commercial Bank (TCB) Sabasaba Moshingi, kwaajili ya kutunisha mfuko wa Tasisi ya Zanzibar Maisha Bora Foundation (ZMBF), wakati wa hafla ya ufunguzi wa Kongamano la Wanawake Zanzibar lililoandaliwa na Tanzania Commercial Bank na kufunguliwa rasmi na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi (kulia kwa Mama) na (kushoto kwa Mama) ni Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa TCB Bw. Edmund Mndolwa.Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi (kushoto), akisalimiana na Katibu wa Baraza la Mapinduzi na Katibu Mkuu Kiongozi Mhandisi Zena Ahmed Said, Mwenyekiti wa bodi ya Wakurugenzi wa Benki ya Tanzania Commercial Bank TCB. Edmund Mndolwa na Afisa Mtendaji Mkuu wa TCB. Sabasaba Moshingi na Mkuu wa Wilaya ya Mjini Bw.Rashid Simai Msaraka,alipowasili katika viwanja vya Hoteli ya Golden Tulip Kiembesamaki kwa ajili ya ufunguzi wa Kongamano la Wanawake lililoandaliwa na Benki ya hiyo katika ukumbi wa hoteli hiyo

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi, pamoja na uongozi kutoka Tanzania Commercial Bank akitembelea maonesho ya Wajasiriamali Wanawake wakati wa Ufunguzi wa Kongamano la Wanawake Zanzibar lililoandaliwa na Tanzania Commercial Bank (TCB), katika ukumbi wa Hoteli ya Golden Tulip Kiembesamaki Jijini Zanzibar leo (kushoto kwa Rais) Mke wa Rais wa Zanzibar Mama Mariam Mwinyi, Katibu wa Baraza la Mapinduzi na Katibu Mkuu Kiongozi Mhandisi Zena Ahmed Said na Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii Wazee Jinsia na Watoto Zanzibar Mhe. Nassor Ahmed Mazrui na (kulia kwa Rais ) Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Benki ya TCB.Bw.Edmund Mndolwa, wakimsikiliza Mjasiriamali Bi. Tatu Suleiman.


Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Benki ya Tanzania Commercial Bank (TCB ), Edmund Mndolwa akizungumza wakati wa ufunguzi wa Kongamano la Wanawake Wajasiriamali Zanzibar lililoandaliwa na Benki hiyo katika ukumbi wa Hoteli ya Golden Tulip Kiembesamaki Jijini Zanzibar.



Afisa Mtendaji Mkuu wa Tanzania Commercial Bank, (TCB), Sabasaba Moshingi akizungumza wakati wa ufunguzi wa Kongamano la Wanawake Wajasiriamali Zanzibar lililoandaliwa na Benki hiyo katika ukumbi wa Hoteli ya Golden Tulip Kiembesamaki Jijini ZanzibarRais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi, akizungumza wakati wa ufunguzi wa Kongamano la Wanawake Wajasiriamali Zanzibar lililoandaliwa na Tanzania Commercial Bank katika ukumbi wa Hoteli ya Golden Tulip Kiembesamaki Jijini Zanzibar



Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi pamoja na Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Benki ya Tanzania Commercial Bank (TCB ), Edmund Mndolwa wakifungua mlango kuashiria uzinduzi rasmi wa Kongamano la Wanawake Zanzibar lililoandaliwa na Tanzania Commercial Bank (TCB) wanaoshuhudia ni Mke wa Rais wa Zanzibar ambae pia ni Mwenyekiti wa Taasisi ya Zanzibar Maisha Bora Foundation (ZMBF), Mama Mariam Mwinyi, Afisa Mtendaji Mkuu wa Tanzania Commercial Bank, (TCB), Sabasaba Moshingi pamoja na uongozi kutoka Serikali ya Zanzibar na Maofisa kutoka Tanzania Commercial Bank





Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akikabidhiwa zawadi maalum ya picha ya kuchora na Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Benki ya Biashara Tanzania (TCB) Bw. Edmund Mndolwa, baada ya ufunguzi wa Kongamano la Wanawake Zanzibar katika ukumbi wa Hoteli ya Golden Tulip Kiembesamaki Jijini Zanzibar leo 5-3-2022, na (kulia kwa Rais) Waziri wa Afrya na Ustawi wa Jamii Wazee Jinsia na Watoto Zanzibar Mhe Nassor Ahmed Mazrui . Mkurugenzi Mtendaji wa (TCB) Bw. Sabasaba Moshingi na Katibu wa Baraza la Mapinduzi Mhandisi Zena Ahmed Said.




No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages