Muonekano
wa hatua iliyofikiwa ya ujenzi wa Daraja la Wami mkoani Pwani. Daraja
hilo lenye urefu wa mita 510 pamoja na barabara unganishi linajengwa kwa
gharama ya shilingi bilioni 67 na linatarajiwa kukamilika mwezi Julai
2022.
Akizungumza
mara baada kukagua maendeleo ya ujenzi wa daraja hilo ambalo ujenzi
wake umefikia asilimia 75.7 Prof. Mbarawa amesema kazi zilizobaki
zifanyike usiku na mchana ili ujenzi huo ukamilike haraka na kwa viwango
vilivvyokusudiwa.
“Daraja
hili lenye urefu wa Mita 510 na barabara unganishi zenye urefu wa
Kilomita 3.8, vyote vikamilike ifikapo Julai mwaka huu,"amesisitiza
Waziri Prof.Mbarawa.
Waziri
wa Ujenzi na Uchukuzi, Prof. Makame Mbarawa akimsikiliza Meneja wa
Wakala wa Barabara (TANROADS) Mkoa wa Pwani, Mhandisi Baraka Mwambage
alipokagua maendeleo ya ujenzi wa Daraja la Wami, mkoani Pwani.
Waziri
Prof. Mbarawa amesema Serikali itaendelea kutoa fedha kwa wakati kwa
miradi yote inayoendelea nchini ili kuwawezesha wakandarasi kukosa
visiingizio vya kuchelewesha miradi nchini na kuwawezesha wananchi
kunufaika na fursa zinazoletwa na miradi hiyo.
“Tumejipanga
kuhakikisha miradi yote ya ujenzi wa barabara, mdaraja na vivuko
inayoendelea inakamilika kama ilivyokusudiwa, hivyo wote mliopata bahari
ya kusimamia miradi hiyo fanyeni kazi kwa uzalengo ilikupata thamani ya
fedha,”amesisitiza Waziri Prof. Mbarawa.
Aidha,
amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe Samia Suluhu
kwa namna anavyowezesha miradi ya kimmkakati ya WIzara ya Ujenzi na
Uchukuzi kutekelezwa na kuitaja miradi hiyo kuwa ni Barabara ya
Bagamoyo-Pangani Tanga hadi Lamu, Daraja la Kigongo-Busisi, barabara ya
mzunguko mkoani Dodoma, Viwanja vya ndege vya Msalato, Mtwara, Musoma,
Songea na Iring ambayo ikikamilika itaibadili sura ya Tanzania kiuchumi
na kijamii.
Mkandarasi
wa Kampuni ya Power Construction Corporation Limited ya China
akimweleza Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Prof. Makame Mbarawa hatua za
ujenzi wa Daraja la Wami, wakati Waziri huyo alipokagua maendeleo ya
ujenzi huo mkoani Pwani. Kushoto ni Meneja wa Wakala wa Barabara
(TANROADS) Mkoa wa Pwani, Mhandisi Baraka Mwambage.
Naye
Meneja wa TANROADS Mkoa wa Pwani Mhandisi Baraka Mwambage amesema
ujenzi wa daraja jipya la Wami lenye upana wa kuwezesha magari mawili
kupishana kwa wakati mmoja utaondoa adha ya daraja la zamani
lililojengwa mwaka 1959 ambalo haliendani na mahitaji ya sasa.
Mhandisi
Mwambage amesema daraja jipya litapunguza ajali na msongamano katika
barabara ya Chalinze hadi Segera na hivyo kuongeza tija kwa watumiaji wa
barabara hiyo.
Waziri
wa Ujenzi na Uchukuzi, Prof. Makame Mbarawa akitoa maelekezo kwa Meneja
wa Wakala wa Barabara (TANROADS) Mkoa wa Pwani, Mhandisi Baraka
Mwambage na Mkandarasi Kampuni ya Power Construction Corporation Limited
ya China wakati alipokagua maendeeleo ya ujenzi wa Daraja la Wami,
Mkoani Pwani.
“Faida
nyingine tunayoipata kutokana na mradi huu ni kuwezesha wataalam wetu
kupata utaalam wa kujenga madaraja makubwa ya kiwango hiki na zaidi ya
wafanyakazi 400 wamepata ajira kulipitia mradi huu,” amesema Mhandisi
Mwambage.
Waziri
wa Ujenzi na Uchukuzi, Prof. Makame Mbarawa akisisitiza jambo kwa
Watumishi wa Wakala wa Barabara (TANROADS) Mkoa wa Pwani, kuhusu
uadilifu na ubunifu katika utendaji mara baada ya kukagua maendeleo ya
ujenzi wa Daraja la Wami, Mkoani Pwani. (PICHA NA WUU).
No comments:
Post a Comment