BONDIA wa ngumi za kulipwa nchini, Ally Ngwando amesema siri ya ushindi wake ni kuzingatia maelekezo ya kocha wake.
Ngwando
ameshinda kwa pointi kwa majaji wote watatu kwa alama 76, 77 na 78
baada ya kumchakaza vikali mpinzani wake, James Kibazange katika pambano
la fainali ya Champion wa Kitaa lililofanyika jana katika Uwanja wa
ndani wa Taifa, Dar es Salaam.
Pambano hilo la utangulizi la kuwania mkanda wa ubingwa wa PST wenye uzani wa kilo 51 raundi nane.
ushindi huo utakuwa chachu ya kuongeza bidii katika mazoezi yake ili kufabya vema katika mapambano mengine.
Ameeleza kuwa ndiyo mara yake ya kwanza kushinda mkanda tangu alipoanza kucheza ndondi.
"Sijamini
pale muandaaji aliposema kuwa ataweka mkanda kati yangu na James
nimwambia kocha nitahakikisha nashinda ili kuwapa furaha mashabiki na
kujiwekea rekodi nzuri, " alisema Ngwando.
Amesema huo ni mwanzo tu atahakikisha anaongeza juhudi ya mazoezi mara mbili zaidi ili kuweka fiti.
Muandaji
wa pambano hilo, Meja Selemani Semunyu amesema pambano la Champion wa
Kitaa limekuwa na mashabiki wengi jambo ambalo hakudhani kuwa hivyo.
Ameeleza
lengo la shindano hilo ni kuibua vipaji vipya ambavyo vipo mtaani
lakini havionekani kwasababu ya mabondia kukosa fursa.
"Huu ni
mwanzo tu wa pambano la Champion wa Kitaa, tulifanya kwa udongo ila
mashabiki watuheshimisha na kulifanya jambo hili kuwa kubwa, naamini
mwakani mambo yatakuwa mazuri zaidi, " alisema Semunyu.
Semunyu
amesema katika pambano hilo wamechagua mabondia watatu waliofanya vizuri
kwa ajili ya kuonyesha burudani nzuri kwa wakazi wa Morogoro katika
pambano la bondia Twaha Kassim 'Twaha Kiduku' dhidi ya Alex Kabangu
kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC).
Katika mtanange
huo pambano kubwa (main Card) lilikuwa kati ya bondia, Maoli Ally dhidi
ya Salehe Mkelekwa, ambapo Maono alishinda kwa TKO.
Baadhi ya
Mapambano mengine ni Said Mkola alishindwa kwa KO dhidi ya Hamad Mkunde,
Selemani Galile alimchakaza vikali Musaa Dragon kwa TKO, Abdallah Pazi
maarufu kama Dullah Mbabe' alimpa onyo kali bondia, Amour Sheikh kwa
kipigo cha KO.
Wengine ni Adam Mbenga alionyesha ubabe kwa kumpiga Hassan Ndonga KO pambano la raundi nane lilimalizika raundi nne.
Bondia wa Ngumi za kulipwa nchini Ally Ngwando mara baada ya kukabidhiwa Mkanda wa ubingwa wenye uzani wa kilo 51 na Mratibu wa pambano hilo Meja Selemani Semunyu katika pambano la champion wa kitaa lililofanyika uwanja wa ndani wa Taifa jijini Dar es salaam
No comments:
Post a Comment