KAMISHNA
wa Uhifadhi wa Shirika la Hifadhi za Taifa Tanzania (TANAPA), William
Mwakilema amewavisha vyeo Makamishna Wasaidizi wa Uhifadhi
waliopandishwa vyeo hivi karibuni.
Tukio hiko limefanyika leo Machi 23, 2022 katika Hifadhi ya Taifa Ziwa Manyara mkoani Manyara.
Waliovalishwa
vyeo ni Kamishna Msaidizi wa Uhifadhi, Fidelis Kapalata na Kamishna
Msaidizi wa Uhifadhi Moses Nonga ambao kabla ya hapo walikuwa Maafisa
Wakuu wa Uhifadhi.
Kamishna
Msaidizi Fidelis Kapalata kwa niaba ya mwenzake ameahidi ushirikiano
kwa viongozi wenzake wa shirika ili kuweza kufikia malengo tarajiwa ya
shirika.Kamishna
Mwakilema amewataka makamishna wapya kufanya kazi zao kwa kuzingatia
viapo vyao, weledi, bidii na maarifa ili kulifanya shirika lisonge mbele
katika majukumu yake ya uhifadhi.
"Ni vema tufanye kazi kama timu moja kwa ushirikiano, tuwe mfano kwa tunaowaongoza pamoja na kuwajengea uwezo wa kushika nafasi za uongozi hapo baadaye,"amesema Kamishna Mwakilema.
No comments:
Post a Comment