Na Rahima Mohamed Maelezo 10/3/2022.
Katibu
Mkuu Wizara ya Afya Zanzibar Dkt Fatma Mrisho amesema hospitali za
kisasa zinazojengwa katika maeneo mbali mbali nchini zitakuwa na vitengo
maalum vya kusafisha damu kwa wagonjwa wa maradhi ya Figo.
Akizungumza
katika siku ya maadhimisho ya siku ya Figo duniani kwa niaba ya Waziri
wa Afya amesema ugonjwa wa figo ni hatari sana hivyo kuwepo kwa kitengo
hicho kutasaidia kuondoa usumbufu wa wagonjwa kufuata huduma katika
hospitali kuu ya Mnazi Mmoja.
Aidha amesema kuwepo kwa kitengo
hicho kitasaidia kuimarisha afya za wagonjwa kwani wanapata usumbufu
mkubwa wakati wanapohitaji matibabu.
Nae Mkurugenzi mtendaji wa
hospitali ya Mnazi Mmoja Dkt Msafiri Marijani amesema endapo wananchi
watabadilisha mtindo wao wa maisha kwa kufuata maelekezo ya wataalam wa
afya wanaweza kuepukana na maradhi tofauti.
Amesisitiza haja ya kufanya mazoezi ya mara kwa mara ili kuweka miili sawa na kuepukana na maradhi nyemelezi.
Kuhusu
tatizo la uhaba wa madaktari bingwa nchini dk. Marijani amewashauri
wataalam na wasomi wa kada ya Afya kusomea fani muhimu ikiwemo upasuaji
mishipa ya damu, moyo, figo ili kupunguza idadi ya kupeleka wagonjwa nje
ya Zanzibar kupata matibabu.
Akisoma risala daktari bingwa wa
ugonjwa wa figo dk.Mariam Hamad amesema wameandaa kampeni maalum ya
kukabiliana na ugonjwa huo hatari ikiwemo kutoa elimu kupitia vyombo vya
habari,vipeperushi na mikutano ya wananchi katika shehia mbali mbali
nchini.
Aidha amesema kitengo chao kinakabiliwa na changamoto
nyingi ikiwemo uhaba wa wafanyakazi, chumba cha upasuaji kwa ajili ya
kusafishia damu na uwekaji vifaa pamoja na mafundi wa mashine
zinapoharibika.
Siku ya figo duniani huadhimishwa kila ifikapo
tarehe 10 Machi ya kila mwaka ambapo kauli mbiu yake kwa mwaka huu ni
“afya ya figo kwa wote”.
Baadhi
ya Wageni waalikwa waliohudhuria katika maadhimisho ya asiku ya Figo
Duniani yaliofanyika katika Uwanja wa Hospitali Mnazi Mmoja Zanzibar.
Msomaji
Risala Dk,Maryam Mohamed Hamad akisoma katika Maadhimisho ya Siku ya
Figo Duniani yaliofanyika katika Uwanja wa Hospitali Mnazi Mmoja
Zanzibar.
Katibu
Mkuu Wizara ya Afya Dk Fatma Mrisho akitoa hotuba ya Maadhimisho ya
Siku ya Figo Duniani yaliofanyika katika Uwanja wa Hospitali Mnazi Mmoja
Zanzibar
Katibu
Mkuu Wizara ya Afya Dk Fatma Mrisho akisisitiza jambo wakati akitoa
hotuba ya Maadhimisho ya Siku ya Figo Duniani yaliofanyika katika Uwanja
wa Hospitali Mnazi Mmoja Zanzibar..
PICHA NA YUSSUF SIMAI/MAELEZO ZANZIBAR.10/03-2022.
Post Top Ad
Your Ad Spot
Friday, March 11, 2022
MAADHIMISHO YA SIKU YA FIGO DUNIANI YAFANYIKA ZANZIBAR.
Tags
KITAIFA#
Share This
About kilole mzee
KITAIFA
Labels:
KITAIFA
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Post Top Ad
Your Ad Spot
No comments:
Post a Comment