A great place to access the latest news and information.

Breaking

Post Top Ad

Your Ad Spot

Friday, March 11, 2022

DIAMOND PLATINUM AIACHIA RASMI FOA EP

 

Na.Khadija Seif, Michuzi TV
ALBUM fupi ya MSANII wa Bongofleva Nasib Abdul maarufu kama Diamond platinum iliyobeba takribani Nyimbo 10 yasikilizwa Kwa mara ya kwanza katika ukumbi wa Terrace slipway jijini Dar es salaam.

Album hiyo iliyobebwa na jina la "Foa" imepokelewa na kuhudhuriwa na Mastaa mbalimbali ndani na nje ya nchi akiwema Msanii Shodmajozi kutoka Afrika kusini.

Katika Nyimbo hizo 10 ameweza kushirikisha wasanii kama Zuchu,Mbosso, shodmajozi na Focalist kutokea nchi Afrika kusini.

Aidha, vibao vinavopatikana kwenye album fupi hiyo ni Nawaza,okoa,Wonder,Fresh,Sana,Mtasubiri,Fine, Somebody pamoja na Melody ambapo Kwa Sasa inapatikana kwenye Mitandao yote ya kupakua Muziki.
Diamond platinum pamoja na Zuchu wakitumbuiza pamoja baada ya kutambulisha wimbo "Mtasubiri" walioshirikiana katika Album fupi "FOA" iliyoachiwa rasmi katika ukumbi wa Terrace slipway jijini Dar es salaam.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages