NAIBU
Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Mary Masanja (Mb) amefunga mafunzo
ya Jeshi la Uhifadhi kwa askari wapya 43 ambao wanajiunga rasmi katika
utumishi wa umma, hafla iliyofanyika kwenye viwanja vya Taasisi ya
Taaluma ya Wanyamapori Pasiansi jijini Mwanza.
Akizungumza
katika hafla hiyo, Mhe. Masanja amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano
wa Tanzania, Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan kwa kutoa ajira kwa vijana
hao.
“Kipekee
nimshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu
Hassan kwa kuwajali vijana na kutoa ajira katika sekta mbalimbali
ikiwemo Sekta hii ya misitu ambapo leo vijana 43 wanapewa fursa ya
kuitumikia nchi,” amefafanua Mhe. Masanja.
Aidha,
amewaasa wahitimu hao kutumia vyema ujuzi na weledi walioupata katika
mafunzo hayo ili kulinda na kusimamia vyema rasilimali za misitu.
Pia,
amewataka kutunza siri za Serikali katika utekelezaji wa majukumu yao
na kuzingatia viapo vya utii kwa Serikali ili kuendelea kuyalinda
maadili na maslahi ya Umma.
Amewakumbusha
wahitimu hao kuwa na utu wanapotekeleza majukumu yao kwa kuepuka
kutumia nguvu pale isipohitahika hasa wanapokutana na wahalifu katika
mazingira yao ya kazi.
Mafunzo
ya Jeshi la Uhifadhi yamefanyika kwa watumishi wa Wakala wa Huduma za
Misitu Tanzania (TFS) yaliyolenga kuwanoa maafisa na askari kuingia
rasmi katika mfumo wa Jeshi la Uhifadhi ili kusimamia vyema rasilimali
za misitu na nyuki.
No comments:
Post a Comment