Na John Walter-Manyara
Kijana
mmoja aliyefahamika kwa jina moja la Said, ameuawa kwa kushambuliwa na
wananchi wenye hasira kali baada ya kudaiwa kumuua mpenzi wake
aliyefahamika kwa jina la Rukia (17-19) mkazi wa kitongoji cha Mbugani
kijiji cha Magugu wilayani Babati mkoani Manyara kwa kumchinja huku
ikidaiwa sababu ni wivu wa Mapenzi.
Baadhi ya Mashuhuda wa tukio hilo wameeleza kuwa wamesikitishwa na tukio hilo kwa kuwa binti huyo alikuwa bado mdogo.
Diwani
wa kata ya Magugu Filbert Modamba amethibitisha kutokea kwa tukio
ambapo amesema chanzo ni ni wivu wa kimapenzi uliotokana na msichana
huyo ambaye kwa sasa ni marehemu kuwa na mahusiano na mwanaume mwingine
baada ya mpenzi wake wa awali kuwa amesafiri kwa muda mrefu ndipo
aliporudi na kumkuta binti huyo na mwanaume mwingine.
Modamba
amesema baada ya tukio hilo, mtuhumiwa alitoroka ambapo jitihada za
kumtafuta zilifanyika na jumatatu Machi 14 wananchi wenye hasira kali
walimpata na kumshambulia hadi kifo chake.
Mwenyekiti
wa kijiji cha Magugu Deogras Ngalawa amesema binti huyo ameuawa kwa
kuchinjwa na kitu chenye ncha kali machi 13,2022 saa tatu usiku.
No comments:
Post a Comment