A great place to access the latest news and information.

Breaking

Post Top Ad

Your Ad Spot

Thursday, February 17, 2022

Tetesi za soka Ulaya Alhamisi

  

_123287270_9bbebb1a-f9a4-4b41-b621-a4415318ad0e

Kiungo mfaransa Paul Pogba, 28, yuko tayari kupokea ofa kutoka klabu zingine za ligi kuu England wakati mkataba wake na Manchester United utakapomalizika mwishoni mwa msimu. (Telegraph)Newcastle inajiandaa kutoa ofa ya £45m kwa ajili ya kiungo mchezeshaji wa Crystal Palace muingereza Eberechi Eze, 23. (Mirror).Nyota wa Manchester United Jesse Lingard, 29 anaweza kukacha kuhamia Tottenham bure mwishoni mwa msimu, kiungo huyo mshambuliaji wa England angetamani kucheza nje ya nchi hiyo (Express).

_123287273_97cdc3e8-89b4-4275-94d4-b7c383711023

CHANZO CHA PICHA,GETTY IMAGES

Rais wa Lyon Jean-Michel Aulas amegusia kwamba klabu hiyo huenda ikamsajili moja kwa moja kutoka kwenye mkopo kiungo mfaransa Tanguy Ndombele, 25 kutoka Tottenham kama klabu hiyo itatwaa kombe la Europa League. (RMC Sport, via Standard).

Winga wa Brazil wa Leeds United Raphinha, 25 ambaye amekuwa akihusishwa na Liverpool, amekataa kusaini mkataba mpya kusalia katika klabu yake hiyo ya Elland Road. (Liverpool Echo)Meneja wa mpito Ralf Rangnick amefanya "usajili" wake wa kwanza kwa kumfahamisha mlinzi wa pembeni Brandon Williams, 21, kwamba atarejea Old Trafford mkataba wake wa mkopo utakapomalizika pale Norwich. (Sun)

_123287274_2edaccae-d438-4e0e-aec5-75f50d849c95

CHANZO CHA PICHA,GETTY IMAGES

Maelezo ya picha,

Ralf Rangnick

Lakini Manchester United huenda ikazuia tena mahitaji hayo ya uhamisho ya Rangnick baada ya kufanya hivyo Januari kwa kiungo mfaransa wa RB Leipzig 24 Christopher Nkunku. (Bild, via Express)Arsenal ni timu ya hivi karibuni ya ligi kuu England kuonyesha nia ya kumtaka mshambuliaji mreno wa AC Milan Rafael Leao, 22. (La Repubblica, via Metro)Newcastle inakabiliwa na mtihani wa kumbakiza mlinzi wake kutoka Uswiswi Fabian Schar, 30 ambaye mkataba wake unaingia katika miezi ya mwisho huku AC Milan, Sevilla na Valencia zikimtaka. (Mail)Brendan Rodgers anasema nyota wa Leicester City Wilfred Ndidi "ana thamani kubwa" zaidi ya £50m baada ya Aston Villa kuhusishwa na kiungo huyo wa Nigeria,25 msimu huu. (Birmingham Mail)

_123287276_bb25ad3c-5585-438f-b6c3-f8678b1a56b8

CHANZO CHA PICHA,GETTY IMAGES

Maelezo ya picha,

Ndidi

Manchester United wanavutiwa kumsajili winga mbrazil wa Ajax Antony, 21 ambaye huenda akaungana na kocha Erik ten Hag pale Old Trafford kama uhamisho huo utazaa matunda. (90min, via Express)West Ham imeungana na Leeds katika mbio za kumsaka kiungo muingereza wa Huddersfield Lewis O'Brien, 23 mwenye kipengele cha thamani ya £12m kwenye mkataba wake. (Teamtalk)

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages