Urusi - ambayo imekuwa ikikana mara kwa mara kupanga kuivamia Ukraine, licha ya kulundika zaidi ya wanajeshi 100,000 karibu na mpaka -inazitaja hofu za mataifa ya Magharibi kuhusiana na uvamizi wake kama "uvumi unaotiwa chumvi ".

Jumatano, wizara yake ya ulinzi ilichapisha video inayoonyesha vifaru vikiondoka Crimea, jimbo ambalo lilitwaliwa na na Urusi kutoka Ukraine mwaka 2014.

Lakini kulingana na afisa wa juu wa White House, maelfu zaidi ya wanajeshi wamewasili katika eneo hilo katika siku za hivi karibuni-ikiwa ni pamoja na siku yenyewe ya Jumatano.

Akizungumza na waandishi wa habari, afisa wa Marekani alikanusha kauli za Urusi kuwa "ilikuwa inaondoa vikosi vyake kutoka kwenye mpaka na Ukraine ".

"Walisikilizwa sana kwa dai hilo, hapa na kote duniani. Lakini tunafahamu ulikuwa ni uongo ."

_118003575_mediaitem118003573

CHANZO CHA PICHA,GETTY IMAGES

Maelezo ya picha,

Mazoezi ya Urusi huko Crimea mnamo Machi 2021 yalizua wasiwasi mkubwa katika nchi za Magharibi

Hii ilikuja saa kadhaa baada ya rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky kuiambia BBC: "Hatuoni kikosi chochote kikiondoka bado, tulisikia tu kuhusu hilo."

Alikuwa akizungumza wakati Ukraine ikiadhimisha kile kinachoitwa siku ya umoja Jumatano,huku bendera za rangu za bluu na manjano zikipeperushwa kote nchini humo.

Rais Zelensky alitangaza siku ya mapumziko ya kupenda nchi baada ya taarifa za kijasusi za Marekani kwamba Urusi inaweza kuishambulia Ukraine siku hiyo.

Katibu mkuu wa Nato Jens Stoltenberg pia amesema kuwa hakuna dalili kuwa vikosi vya Urusi vimeondoka, akisema Jumatano kwamba tisho kutoka kwa Urusi limekuwa "jambo jipya la kawaida ".

Akizungumza katika mkutana wa mawaziri wa ulinzi wa Nato mjini Brussels, Bw Stoltenberg alisema muungano huo unaangalia uwezekano wa kupanga makundi mapya ya mapigano, aina ndogo zaidi ya vikosi vya kijeshi vyenye uwezo wa kujisimamia -katika Ulaya ya kati na Kusini magharibi mwa Ulaya.

Alisema hii ni sehemu ya hatua zinazoendelea za kuimarisha ulinzi wa Ulaya - ambapo dola bilioni 270 (pauni bilioni 199 ) zimetumika tangu mwaka 2014-ingawa alijaribu kuihakikishia Urusi kwamba Nato sio tisho.

Ufaransa ilijitolea kuongoza moja ya kikundi cha mpigano katika Romania, alisema.

Wizara ya mambo ya nje ya Urusi ilisema "haina haja tena" na kauli za Bw Stoltenberg.

_123222252_drill

CHANZO CHA PICHA,EPA/RUSSIAN DEFENCE MINISTRY

Maelezo ya picha,

Maelfu ya wanajeshi wa Urusi wamekuwa wakifanya mazoezi ya pamoja ya kijeshi huko Belarus, ambako kuapakana na Ukraine

Kutoaminiwa kwa dai la Urusi la kuondoa wanajeshi wake ni jambo lililoungwa mkono na wazri mkuu wa Uingereza Boris Johnson ambaye alimwambia katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa kwa njia ya simu kwamba kuna "dalili ndogo sana kwa sasa za Urusi kuondoa vikosi vyake", huku mkuu wake wa ujasusi wa ulinzi Luteni -Jenerali Jim Hockenhull akisema kwamba, kinyume chake , Urusi inaendelea kuongeza idadi ya vikosi vyake.

"Hii ni Pamoja na kuonekana kwa magari ya kijeshi zaidi, helikopta na hospitali za dharura zinazohamishwa kuelekea kwenye mipaka ya ukraine," alisema. "Urusi imewalundika wanajeshi wake ili Ukraine."

    Jumatano, Wizara ya mambo yan je ya Marekani ilionya kwamba maafisa wa Urusi wanatunga hadithi katika vyombo vya habari zenye lengo la kushawishi 'maoni ya umma pale utakapofanyika uvamizi.

    Msemaji wa wizara hiyo Ned Price alielezea hofu juu yad ai la Bw Putin kwamba - "mauaji ya halaiki" yalifanyika mashariki mwa Ukraine.

    Wakati huo huo , maafisa wa Urusi, walisema kuwa wanachunguza madai ya makaburi ya watu wengi ambayo yana mamia ya raia katika eneo la mzozo.

    Urusi na Ukraine zina uhusiano wa muda mrefu wa kitamaduni na kihistoria, nan chi zote mbili zilikuwa sehemu ya Muungano wa Usovieti.

    Rais wa Urusi Vladimir Putin anataka hakikisho kwamba Ukraine haitajiunga na Nato kwasababu anaona upanuzi wowote wa muungano huo kama tisho kwake. Nato imekataa dai hilo.

    Mapema wiki hii, Bw Putin alisema kwamba Urusi haitaki vita, lakini akadai kwamba suala ya uanachama wa nato litatuliwe sasa, hatakama Ukraine bado ina njia ndefu ya hata kuanza maombi ya kujiunga na muungano wa Nato.

    Ramani inayoonyesha kupanuka kwa muungano wa Nato tangu mwaka 1997:

    _122647781_nato_member_states_10jan_map640-2x-nc